- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imeipatia shilingi milioni 265 shule ya sekondari ya Murusagamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa ajili ya kujenga Bweni, Maktaba, Bwalo na jiko, pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo, ambayo ina kidato cha kwanza hadi cha sita.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Februari 13, 2019 ofisini kwake; Afisaelimu Idara ya Sekondari Ndugu Fikeni Ezekiel Senzighe, na kuwataka kamati ya ujenzi, bodi ya shule pamoja na wadau wote wa elimu washirikiane, ili wakamilishe zoezi hilo.
“Fedha hizi zimegawanyika katika miuondombinu ifuatayo shilingi milioni 100 zitajenga Bwalo, shilingi milioni 75 zitajenga Bweni, shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga Maktaba, na shilingi milioni 40 zitatumika kujenga vyumba 02 vya madarasa.” Alisema Ndugu Senzighe.
Aidha, amesema kamati ya ujenzi na bodi ya shule hiyo, kujitolea nguvu zao, ili tuweze kutekeleza ule mradi jinsi unavyotakiwa hata na zaidi, kwa maana kwamba zipokata nyingi zenye sifa, lakini hawajapata hii bahati.
Miradi hiyo itatekelezwa kwa kutumia false akaunti, ambayo inatumika katika ujenzi wa miundombinu ya serikali katika shule za sekondari na za msingi, huku akisema wamafika shuleni kutoa elimu kwa kamati na Bodi ya shule namna ya kutumia fedha hiyo.
Idara ya elimu sekondari na timu ya wataalamu wa Halamashauri ya Wilaya ya Ngara watafanyakazi pamoja na kamati hiyo, kwa ajili ya kutoa ushauri na usimamizi wa kitaalamu pale watakapohitajika kufanyahivyo wako tayari.
“Hadi sasa kamati ya ujenzi na bodi ya shule wamewezeshwa namna watakavyofanya matumizi, matangazo yamesambazwa, kwa ajili ya kupata mafundi; na kwamba ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imewaandikia barua rasmi ya maelekezo jinsi ya kutumia fedha.” Alisema Ndugu Fikeni.
Ameonya sheria inasema wazi kwamba mtu atayekiuka sheria za manunuzi; kwa maana kwamba atasababisha uharibifu wa fedha ya umma, au atafanya matumizi visivyo halali, lazima sheria ichukue mkondo wake, huku akidai kwamba watafanya usimamizi wa karibu ili hali hiyo isijitokeze.
Shule ya sekondari ya Murusagamba ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita; ambapo shule hiyo ina mchepuo wa masomo ya sayansi; na wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao ya ndani, kiwilaya, kimkoa na hata kitaifa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa