- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwekezaji wa Kampuni ya Tripp Co. Ltd kutoka nchini Korea Kusini Ndugu Kim Un, ametembelea eneo la ekari 1000, lililoko katika kata ya Keza eneo la Msalasi na Muko, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa ajili ya kuwekeza katika zao la kahawa na viwanda vya kukoboa kahawa na kutengeneza mbolea.
Akimuonyesha eneo hilo Mei 13, 2018, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amemwambia kwamba Halmashauri yake inayo ardhi ya kutosha, kwa ajili ya shughuli za kilimo na kwamba atapata ardhi anayoitaji kwa ajiili ya shughuli zake.
Ndugu Bahama alimwambia mwekezaji huyo. kwamba eneo alilompatia ni la kimkakati. kwani Tanzania inajenga reli ya kisasa itakayopitia eneo hilo kwenda nchini Burundi na Rwanda, itakayosaidia kusafirisha bidhaa zake, na kuongeza kwamba kuna mradi wa umeme wa maji utakotumika katika viwanda atakavyoanzisha.
“La msingi mtuandikie mahitaji yenu ya ardhi mnayohitaji; kwa sasa tuna hizo ekari 1000, lakini tunaweza kupata zaidi ya hizo, hivyo ardhi inayoongezeka tutawapa tu bila wasiwasi.”alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Muwekezaji huyo baada ya kupata eneo hilo alilidhika, na kusema kwamba mbali na kuwekeza katika zao la kahawa angependa kupata ekari 4000, kwa ajili ya zao la kahawa, ekari 4000 kwa ajili ya kulima mpunga, na ekari 4000 kwa ajili ya kuwekeza katika mbegu za viazi mvilingo.
“Lengo kubwa ni kuanzisha mradi wa mashamba makubwa ya kahawa aina ya Arabika, si kwa ajili ya Tanzania na Afrika tu bali kwa dunia nzima, lakini pia nataka kuanzisha shamba la viazi kwa ajili ya mbegu na mradi wa kilimo cha mpunga utakuja baadae.”alisema Ndugu Kim Un.
Mwekezaji huyo ameahidi kushirikiana na wananchi na kuwaomba wajiandae kulima kahawa, kwani yeye atainunua kahawa yao na kuwapa ajira katika mashamba yake ya kahawa, na katika viwanda atakavyoanzisha.
Aidha, amesema atahakikisha huduma za jamii kama vile maji, shule na zahanati zinajengwa, kwa kushirikiana na wananchi hao; huku akidai kwamba wananchi hao watajifunza teknolojia mpya ya kuzalisha zo la kahawa.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka, amewataka wananchi kushirikiana na mwekezaji huyo, kwa madai kwamba mwekezaji anapowekeza wananchi wanafaidika, kwa ajira na kuuza mazao yao.
Ndugu Tibaijuka amewahakikishia, kwamba ikiwa kuna wananchi ambao ardhi yao itakuwa katika eneo alilopewa mwekezaji, watalipwa fidia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri atalishughulikia hilo kwa kuweka makubaliano yote katika maandishi.
Mwekezaji huyo, aliambatana na Maratibu wa Mratibu wa mradi nchini Korea ndugu, William Mwingira, Waratibu wa Mradi nchini Tanzania ndugu David Mabura, Ndugu Daniel Ndayanse, Ndugu Karim Amri na Ndugu Issa Samma.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa