- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Tarehe 29/02/2024, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii amefanya Ziara katika Wilaya ya Ngara kwa lengo la Kusikiliza na Kutatua KERO za Wafugaji hususani wa Kata ya Kasulo ambayo sehemu kubwa inapakana na Hifadhi ya Burigi - Chato.
Naibu Katibu Mkuu CP Benedict Wakulyamba katika Ziara yake alifuatana na Viongozi mbalimbali toka Makao Makuu ya TANAPA, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi - Chato, Mhe Col. Mathias Julius Kahabi DC Ngara, Ndg Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi. Hatujuani Ally Lukari katibu Tawala Wilaya pamoja na Kamati ya Usalama ya Wilaya.
Naibu Katibu Mkuu CP Wakulyamba amefanya Mkutano wa Hadhara uliohudhuliwa na Wafugaji na Viongozi wa Chama na Serikali wa Kata ya Kasulo akiwemo Diwani wa Kata hiyo Mhe. Yusuph Katura pamoja na Diwani Viti Maalum Mhe. Zawadi Cosma.
Aidha, wafugaji walipata nafasi ya kuuliza maswali na KERO mbalimbali ambazo kwa ujumla zilijibiwa kwa ufasaha na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye eneo la mkutano wa Hadhara Kata ya kasulo.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya MALIASILI na UTALII CP Benedict Wakulyamba akiongea na wananchi Wafugaji Kata ya Kasulo.
Wananchi Wafugaji waliojitokeza katika mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya MALIASILI na UTALII kusikiliza na kutatua kero za Wafugaji Kata ya Kasulo.
Naibu Katibu Mkuu akiwa na Mhe Kanali Mathias J Kahabi , Ndg Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Bi Hatujuani A Lukali na viongozi wengine katika mkutano wa hadhara (Wafugaji) Kata ya kasulo.
Kazi iendelee..........
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa