- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amepiga marufuku kwa wakulima kuuza mazao kwa kutumia lumbesa.
Kigahe amepiga marufuku hiyo kwa wakulima na wafanyabiashara desemba 20,2023 wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Njombe.
Naibu Wazi huyo amesema kuwa ni wakati sasa kwa wakulima kuanza kuuza mazao yao ya kilimo kwa vipimo vilivyoelekezwa na serikali kupitia wakala wa Vipimo (WMA) na kuacha kutumia lumbesa ambapo inampa hasara mkulima pamoja na Serikali kukosa mapato yake.
Kigahe amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara imeanza mkakati Kwa kuunda kikosi kazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Kilimo pamoja na baadhi ya wafanyabiashara ili kupata taarifa na takwimu za wapi biashara za lumbesa zinafanyika kwa Nchi nzima ili kuweka uelewa wa pamoja wa namna ya kuwasaidia wakulima kuacha kuuza mazao kwa njia hiyo.
Vilevile Mhe.Kigahe amewataka wakulima wote Nchini kuacha kuuza mazao yao shambani badala yake wajiunge kwenye vyama vya ushirika ambavyo vitasaidia kupata masoko ya uhakika na kupanga bei elekezi za mazao kwa Pamoja.
Aidha Naibu Waziri amesema kuwa ili kuwasaidia wakulima ni wakati sasa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanaanza kuandaa sehemu za kuuzia mazao kwa pamoja ili kuepusha uuzaji wa mazao kwa mtu mmojammoja na kama Wizara kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) tutatoa mizani ili kusaidia upimaji.
Aidha, Mhe.Kigahe amelitaka Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuanzisha tuzo maalum kwa wabunifu ili kuongeza chachu ya ubunifu na uzalishaji nchini
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa