- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe Mhandisi Kundo Andrea Methew amekagua ujenzi wa kituo kipya cha Mkongo wa Taifa Cha Rusumo chenye thamani ya Shilingi Bilioni 1,091,722,840.24. Mhe. Kundo amewaeleza wananchi wa Rusumo kuwa tatizo la mawasiliano katika mpaka huo wa Tanzania na Rwanda sasa limefika mwisho. Amesema
"Serikali ipo katika mchakato wa mwisho wa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa minara mingine 636 na minara 15 itajengwa katika maeneo ya mipaka kwa ajili ya kuboresha usikivu wa Radio na minara 621 itajengwa kwa ajili ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu Nchi nzima"
Pia Naibu Waziri Kundo akizungumza na wananchi wa Rusumo ameeleza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amenunua magari 45 yenye thamani ya Shilingi Bilioni saba yatakayo saidia katika utekelezaji wa huduma za mkongo Nchini.
Ambapo Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe. Col. Mathias Julius Kahabi ameipongeza serikali kwa kupatiwa billioni 38.5 kwa ajili ya maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu ya Barabara Umeme na Mradi wa uchimbaji wa Madini TEMBONIKEL Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya ya Ngara mbele ya ya Naibu waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Methew katika ziara yake Rusumo wilayani Ngara.
Kwa upande wake Mhe Methew amemupongeza Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe George Ndaisaba Ruhoro kwa kazi nzuri ya kuhamasisha maendeleo hasa kwa kushirikiana na serikali pamoja na wananchi katika sekita ya mawasiliano na amewasa wananchi wa wilaya ya Ngara kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yao hasa ya kiuchumi na kijamii na kuepukana matumizi yasiyo kuwa ya tija katika jamii.
Katika ziara hiyo , Mhe. Mbunge wa Ngara ameishukuru serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Kwa jitihada za kuhakikisha mawasiliano katika wilaya ya Ngara yana imarika hususani kata ya Rusumo pia amempongeza DC, DED pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Ngara kwa kutoa ushirikiano wa kusimamia miradi mbali mbali hadi kukamilika kwa miradi hiyo.
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Kundo A Mathew akisalimiana na viongozi mbalimbali Wilayani Ngara.
Wananchi katika mkutano wa hadhara wa Mhe Naibu Waziri.
Mhe Naibu wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akiwa na Mhe Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G Ruhoro.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa