- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Natamuka rasmi kwamba pikipiki ya serikali aipotei wala kuibwa; itakayopotea au kuibwa ni pikipiki binafsi ya Afisaelimu Kata.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama.
Ndugu Bahama, ameyasema hayo wakati akipokea pikipiki 22, kofia ngumu 22 na ‘groves’ 22, vilivyopokea toka Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia Septemba 07, 2018 kwa lengo la kuwasaidia Mafisaelimu Kata kusimamia ubora wa elimu katika Kata zao.
Ndugu Bahama amesema serikali imetoa pikipiki hizi kwa Maafisaelim Kata, ili waweze kusimamia ubora wa elimu kupitia mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu KKK.
“Kama zilivyo Halmashauri nyingine hapa nchini ambazo zilikuwa na tatizo la watoto wa shule za msigni kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu, Halmashauri ya Ngara nayo bado inachangamoto hiyo, lakini naamini pikipiki hizi zitakuwa msaada mkubwa katika kutokomeza tatizo hili.” Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji Ndugu Bahama.
Alisema kuwa wanapokea pikipiki hizo kama sehemu ya serikali katika kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014, inayomtaka mtoto wa kitanzania amalizapo elimu ya msigi awe na maarifa, mahiri, na uwezo wa kuleta maendeleo yake binafsi na ya taifa.
Ndugu Bahama anaishuskuru serikali kwa kuamua kutoa pikipiki hizo alizosema, kwamba ni mbinu mbadala zitakazowasadia maafisaelimu kata, kusimamia kwa karibu suala la kusoma, kuandika na kuhesabu ili watoto wanaohitimu darasa la saba waweza kufaulu mitihani yao ya ndani na hata ya kitaifa.
Aidha, anapongeza juhudi za serikali katika kuinua ubora wa elimu hapa nchini pamoja na walimu huko shuleni, kwani mpango umeishaanza kuzaa matunda, kwani watoto wanaohitimu shule wengi wao wanaweza kusoma, kuandika na hata kuhesabu; ilikilinganishwa na miaka mitano iliyopita.
Amewaonya Maafisaelimu Kata wanaokwenda kuzitumia pikipiki hizo, kwamba vitendeakazi hivyo ni mali ya serikali si mali binafsi; hivyo hategemei kukuta vinafanyakazi kinyume na malengo na maelekezo ya serikali.
Akifafanua jinsi usafiri huo utakavyowasaidia katika utendaji kazi wao, Afisaelimu Kata ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema kwamba pikipiki hizo si msaada kwa watoto wa shule za msingi, tu bali hata katika majukumu mengine katika kukuza ubora wa elimu nchini.
Amesema pamoja na kufuatilia suala la KKK, bado atakuwa na nafasi ya kufuatilia masuala ya elimu, aliyoyataja kuwa ni maandalio ya masomo, mahudhurio ya wanafunzi na utendajikazi wa walimu katika shule za msingi na za sekondari katika kata zao.
“Itakuwa ni ajabu nifike shuleni nifanye jambo moja la KKK, wakati shuleni hapo kuna matatizo mengine, au nishindwe kufuatilia utendajikazi wa walimu katika shule ya sekondari ilipo katika kijiji hicho hicho.” alisema Afisaelimu kata huyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa