- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers Cooperative Society LTD (NFCSL) hadi September 09, 2018, kimekusanya kilo 952,056 za kahawa aina ya Arabika, na kuwalipa wakulima jumla ya shilingi 939,726,000.
Hayo ni kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers Cooperative Society LTD Ndugu Amphrey S. Kachecheba, wakati akiwasilisha taarifa ya makusanyo ya kahawa msimu wa 2018/2019 mjini Dodoma.
“Msimu huu tulitarajia kukusanya tani 2,000 za kahawa kutoka kwa wakulima Wilayani Ngara, ambapo Arabika tilikisia tani 500 na Robusta tani 1,500; lakini hadi katikati ya mwezi wa tisa tumekusanya kilo zipatazo 952,056.” Alisema Ndugu Kachecheba.
Amesema kwao hayo ni mafanikio kwani Chama cha Ushirika kimeongeza kilo zipatazo 452,056, ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 90.4; ingawa bado chama kinadaiwa kiasi cha shilingi 12,330,000/= sawa na kilo 12,330.
Aidha, ameogeza kwamba hadi Septemba 09, 2018, wamefanikiwa kukoboa magunia yapatayo 629, kati ya hayo magunia 561, yamewekwa kwenye madara tofauti aliyoyataja kuwa ni FAQ, UG, TRIAGE, NA BHP.
Mafanikio mengine aliyoyataja Ndugu Kachecheba ni kwamba, wakulima wengi wanauza kahawa iliyosafi na bora baada ya kuelimishwa na chama hivyo, kuanika kahawa yao kwenye chanja na maturubai.
Amezitaja changamoto zinazokikabiti chama hicho, kuwa ni baadhi ya mashine zao za kukoborea kahawa kuaharibika vipuri, kwa sbabu ya kukaa muda mrefu bila kufanyakazi.
Kukatika mara kwa mara kwa umeme, amsema kunakwamisha shughuli za kukoboa kahawa na hivyo kusababisha mlundikano wa kahawa katika maghala machache waliyonayo, hivyo kulazimika kuahifadhi kahawa hiyo nje.
Ukosefu wa maghala ya kuhifadhia kahawa kwao ni changamoto, kwani msimu wa mvua unakaribia, na kuuomba uongozi wa wilaya kutafuta njia ya kutatua changamoto hiyo, na kuongeza kwamba maghala yamechakaa sana kwani yamekaa muda bila kukarabatiwa.
Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers hakijabweteka, bali kimechukua hatua ya kukodisha mashine za kiwanda cha Ngara Coffee; kama mbadala wa kukoboa, kuchambua na kuweka madaraja mbalimbali ya kahawa.
Chama kimeendelea kushirikiana na na vyama vikuu vya ushirika mkoani Kagera, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, pamoja na Wizara ya Kilimo, katika kutatua matatizo na kujifunza uzoefu katika suala zima la ukusanyaji, kuhifadhi, kukoboa na kutafuta soko la kahawa.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidani Bahama, amewataka wanachi kuwa nasubira, wakati serikali inatafuta ufumbuzi wa matatizo yao ya malipo ya kahawa.
Amewafafanua kwamba Chama cha Ushirika kintarajia kupeleka sampuli ya kahawa ya wakulima, iliyowekewa madaraja na baada ya sampuli hiyo, kutoka mnadani wataweza kufahamishwa bei kamili kwa kilo moja ya kahawa.
Wakulima walitaka kujua kama watarejeshewa magunia yaliyochukuliwa na chama hicho wakati wanauza kahawa yao, Meneja wa Chama cha Ushirika Ndugu Kachecheba amewahakikishia wakulima hao, kuwa chama kitwarejeshea magunia yao pindi yatakapopatikana.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa