- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Benki ya Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), imekikopesha Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers’ Co-operative shilingi bilioni moja milioni mia tano (1,500,000,000/=), kwa ajili ya kununua kahawa katika msimu wa 2017/2018.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Ngara ndugu Gonashi Levinus Kulwa, amesema haya Machi 20, 2018 ofisini kwake, kwamba TADB imekubali kutoa kiasi hicho, baada ya kujiridhisha kuwa Ngara Farmers’ Co-operative, wamejipanga kuanza kununua kahawa msimu huu.
“Tunatarajia kuanza kununua kahawa kuanzia Mei 2018, kwa kununua kahawa aina ya Arabika kwanza, na tutanunua Robusta hapo baadae.” Alisema Ndugu Kulwa.
Amewahasa wakulima kutumia nafasi hiyo kujiinua kiuchumi, kwani fedha ipo tayari na mikataba imekamilika na kudai kuwataka wasiipoteze fursa hiyo.
Amewaonya wakulima waache tabia ya kuuza kahawa kwa walanguzi, kwani kufanya hivyo ni kukirudisha nyuma, na kukikwamisha chama hicho cha ushirika.
Amesema kwamba wamepata mkopo huo, baada ya ziara ya Waziri wa Kilimo na Ushirika Mhe. Charles Kizeba wilayani Ngara mwezi Februari 2018, na kuwaahidi wanachama wa Ngara Farmers’ Co-operative, kwamba atawatafutia mkopo wa kununua kahawa katika msimu huu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa