- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoa wa kagera imeanza wiki ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara
Maadhimisho yameanza tarehe 04/12/2026 Kwa kupamba Ofisi za Serikali Kwa Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ,Ambapo kumewekwa picha ya Rais wa Kwanza Mwalimu Julius K. Nyerere na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
Wananchi ,watumishi Mbalimbali hufika katika eneo lililopambwa na kusaini kitabu Cha kumbukumbu ya Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru Wa Tanzania Bara.
Maadhimisho yataendelea Hadi tarehe 9/12/2023 Kwa matukio Mbalimbali kulingana na ratiba ya Maadhimisho.
Aidha katika maadhimisho hayo yataendana na shughuli zifuatazo kusaini kitabu Cha kumbukumbu, kufanya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, kuongea na wazee maarufu , kufanya usafi kabambe , kupanda miti zaidi ya 1,380, Uchangiaji damu , matembezi ya kilometa 5 na kufanya mazoezi ya pamoja Aerobic, michezo ya kukimbiza kuku, kuvuta kamba , kukimbia na chupa yenye maji kichwani na Mdahalo/kongamano.
Katika maadhimisho hayo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi .
Kauli mbiu ya Maadhimisho ni UMOJA NA MSHIKAMANO NI CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA LETU.
Watumishi wakisaini kitabu Cha kumbukumbu ya wiki ya Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru kiwilaya.
Afisa Utumishi Wilaya Bi Sabra Mwankenja.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa