- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imefanikiwa kujenga kituo kipya cha Afya cha Rusumo kinachopatikana kata ya Rusumo. Kituo hicho kinaenda kuongeza idadi ya vituo vya Afya wilaya ya Ngara na kuwa jumla ya vituo vya Afya vitano (05) yaani Murusagamba, mabawe, Bukiriro na Lukole. Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngara Ndg. Solomon kimilike alisema kituo hicho kina ukumbwa wa hekari 6.32 na ujenzi ulianza mwezi Mei 2020 kwa ufadhili wa Benk ya Dunia (World Bank) kipitia wakala wake NELSAP ( Nile Equatorial lake Subsidiary Action Program).
Aidha aliendelea kwa kusema mradi una majengo 14 yakijumuisha OPD,Wodi ya Wazazi, Maabara, Wodi na majengo mengine yamuhimu katika kituo cha Afya. Gharama za mradi zilizotumika mapka sasa ni Tsh 1,328,888,674.62. Mradi ukikamilika utahudimia wananchi wapatao 15,500 wa kata za Rusumo, Murukulazo, Kasulo na kata zingine za jirani.
Kuwepo kwa kituo hiki kitaondoa adha kubwa waliokuwa wakiipata wananchi kufuata matibabu zaidi ya kilomita 21 kufuata huduma hospitali za Murgwanza na Nyamiaga zinazopatikana makao makuu ya wilaya.Shughuli zilizobaki ni kujenga uzio, kuunganisha huduma ya maji, umeme,maboreho ya Barabara kwa kiwango cha changalawe,vifaa tiba,samani za ndani, kujenga placenta pit, Mkakati wa kikamilisha umepangwa kutekeleza kupitia awamu ya pili ya mradi wa LADP .
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa