- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amepokea Ugeni wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Biashara kwa kufungua Kikao cha Kamati hiyo na Wafanyabiashara katika Mpaka wa Tanzania na Burundi(Kabanga OSBP) tarehe 17/7/2024.
Kamati hiyo inaongozwa na Mhe Balozi Dr. John S. Simbachawene - Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Wajumbe wengine ni pamoja na Dr. Ashura A. Katunzi - Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw. Juma Hassan Bakari - Kamishna wa Forodha TRA, Afande CP Awadh Juma Haji - Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, Bi. Angela Shija - Kamishna wa Uhamiaji, Bw. Mbayani Y. Saruni - Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Dr. Edgar Mahundi - Mkurugenzi TMDA, Bw. khamis Ahamada Shauri - Mkurugenzi Wizara ya Biashara Zanzibar, Bw. Ombeni Mwasha - Mkurugenzi Wizara ya Viwanda na Biashara na Wajumbe wengine wanaunda Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Biashara.
Lengo la Ziara hiyo ni kuongea na Wafanyabiashara wa maeneo ya mpakani, kupata taarifa za Biashara zinazofanyika maeneo ya mpakani, kusikiliza KERO na Changamoto zilizopo kwenye maeneo ya mpakani na kuzitolea majibu ya Serikali.
Aidha, Kamati hiyo Iliendelea na majukumu yake Tarehe 18/7/2024, kwa kutembelea Mpaka wa Tanzania na Rwanda(Rusumo OSBP).
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa