- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wananchi nataka niwe wazi, fedha toka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi, nitazipeleka kwa wananchi wanaochangia miradi ya maendeleo.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan J. Bahama.
Ndugu Bahama aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji cha Nyarulama katika Kata ya Kibogora Wilaya ya Ngara, wakati akiwahamasisha wananchi kuhusu umhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo.
Amewapongeza wananchi hao kwa kutumia nguvu zao kukakamilisha maboma mawili ya jengo la zahanati na ofisi ya kijiji; kwa kuridhishwa na juhudi hizo, Mkurugenzi Mtendaji amewaahidi kuwapatia mabati ya kukamilisha majengo hayo.
Amewaomba wananchi ambao wanasuasua katika kuchangia miradi ya maendeleo kijijini hapo, kuacha mara moja tabia hiyo kwani haijengi, na kuwataka wajiunge na wenzao katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji huyo amewakumbusha wananchi kuchangia shilingi 30,000/=, kwa ajili kupata kadi ya Bima ya Afya, ambayo amesema itawasaidia kutibiwa katika zahanati yao hadi hospitali ya rufaa ya mkoa.
Amesema kadi hiyo inawarahisishia maisha kwani gharama za matibabu kwa mtu asiyekuwa na bima ya afya ni kubwa, ambayo mtu mmoja mmoja inakuwa vigumu kuzimudu, lakini wakiwa na bima ya afya; gharama hizo zinapungua maradufu.
Wananchi walitaka kujua ni lini wataanza kuchangia fedha hiyo, kwani wengine walikuwa tayari wameiskusanya na wanaongopa kuitumia, kwani kila walipokuwa wakimpelekea mganga katika zahanati yao alikuwa anawataka waendelee kusubiri.
Ndugu Bahama amewaambia utaratibu bado haujaletwa wa jinsi ya kukusanya fedha hiyo hivyo akawashauri wawe na subira wakati serikali ikifanya mchakato wa kukusanya fedha ya bima ya afya.
Naye Diwani wa Kata ya Kibogora Mh. Adronizi Burindoli amesema pamoja na kufanikiwa katika kukamilisha maboma hayo, bado kata yake ina changamoto za ukosefu wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya watoto wa awali na wa darasa la kwanza.
Mh. Bulindori amesema baada ya kutangazwa kwa elimu pasipo malipo mwitikio wa wananchi, kuwaandikisha watoto umekuwa mkubwa, matokeo yake watoto walioanza darasa la kwanza na awali wameongezeka mara dufu na kupelekea upunfu wa vitendea kazi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa