- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo hayo yanatolewa Kwa Wakuu wa Idara na Vitengo 18, Wasaidizi wa Wakuu wa Idara na Vitengo 18 na Wakuu wa sehemu (section) 26 Toka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Mafunzo hayo yatafanyika Kwa siku Mbili tarehe 11/12 Hadi 12/12/2023 katika ukumbi wa St. Fransis Ngara Mjini.
Mafunzo yanaongozwa na timu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma Bi Jeanfrida B. Mushumbuzi Mkurugenzi Msaidizi Toka Ofisi ya Utumishi na wengine ni Ndg Edson L. Mwakufamba, Bi Mary D Lisakafu, Bi Naomi c.Rutaihwa na Bi Ester komba.
Mafunzo yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike Kwa kusisitiza mafunzo hayo ni Muhimu sana kuwepo wote bila Uwakilishi ,kusikiliza Kwa Makini ili kazi ya kuingia kwenye mfumo iweze fanyika vizuri.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa katika mafunzo ya PEPMIS,PIPUMIS NA HR ASSESSMENT katika ukumbi wa St Francis.
Viongozi wakiwa katika mafunzo.
Mafunzo yakiendelea katika ukumbi wa St Francis Ngara Mjini.
Wakuu wa Idara ,Vitengo na Wasaidizi wao wakiwa katika mafunzo.
Viongozi wakisikiliza Kwa Makini mada iliyotolewa dhana ya usimamizi na utendaji kazi katika utumishi wa Umma.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa