- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Naamini kwa umri wenu mnaweza kusonga mbele kimichezo mradi muwe na nidhamu ya kufanya mzoezi, na kuachana na mambo yasiyojenga katika maisha.” alisema makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Geogia Munyonyera.
Bi Mnyenyera ameyasema hayo Oktoba 11, 2018, katika Kata ya Ngara Mjini katika Mtaa wa Mukididili, wakati akikabidhi jozi 25 kwa timu za Ndole na Mukatanga.
“Leo tunategemea mtaonyesha mchezo mzuri tuone, lakini lego ni kuwakutanisha, ili muendelee kuwa na undugu, urafiki na maelewano; maana mnapokutana mnafahamiana zaidi.” alisisitiza Bi. Munyonyera
Aliwaambia wachezaji hao, kwamba michezo ni afya, ni upendo na ni ajira, akawataka waendelee kumwomba Mwenyezi Mungu, awape nguvu tele waweze kufanikisha nia njema waliyoianza ndani mwao.
Aidha, amewataka kuzitunza jezi hizo, ili ziweze kufanikisha kile walichokusudia huku akiwataka kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mtaa wao Bi Faidhi Rugambati aliyemuomba Bi Munyonyera kuwafadhili jezi hizo.
Amesema kwamba hakukurupuka kufahdili timu hizo, bali baada ya kupata wazo hilo, allilipeleka katika vikao mbalimbali vya kata vya Mtaa, kitongoji na hata kijiji, apate Baraka kutoka kwa uongozi.
Mmoja wa akina mama aliyehudhuria katika hafla hiyo, alinukuliwa akisema kwamba anamshukuru Bi. Munyonyera kwa ufadhiri huo, kwani kwa kuwashangilia vijana wao amepata muda wa kucheka na kutaniana na wenzake.
Vijana wameahidi kuhudhuria mazoezini kila jioni, ili wajiendeleze kimichezo, huku wazee wakisema wamepata mahali pa kupotezea muda wakati wa jioni, badala ya kukaa kwenye vilinge vya pombe.
Baada ya kupata jezi timu zilitunishiana misuli ambapo Ndole FC; iliibuka kidedea kwa kuifunga Mukatanga FC mabao mawili kwa nunge, ambapo magoli ya Ndole FC yalifungwa na Alon Rugondoka na Emmanuel Agonda.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa