- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kanali Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara Tarehe 23/12/2023, akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Solomon Kimilike pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kata ya Rusumo.
Mhe. Mkuu wa Wilaya akiwa na viongozi hao walitembelea Mradi wa Ujenzi na ukarabati wa Nyumba za Waathirika wa blasting unaotekelezwa na Wakandarasi wawili wa Kampuni za Azhar Company Ltd na Kika Company ambapo maendeleo ya Ujenzi na ukarabati huo unaendelea vizuri.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanali Mathias Kahabi na Kamati yake ya Usalama wameridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi na ukarabati huo na kuwataka Wakandarasi hao kuongeza speed ya ujenzi. Aidha, amewataka Wakandarasi hao kushirikiana kwa karibu na Wananchi Waguswa wa Mradi huo kwa kuwashirikisha kila hatua bila kuacha malalamiko ya aina yoyote na kwamba asiluuzwe Mwananchi anapokuwa anahoji Jambo lolote ikiwemo kujua stahiki zao na malipo mengine wanayotakiwa kuyapata toka NELSAP ambao ni wasimamizi wa mradi huo.
Aidha akiwa katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza KERO za wananchi Mhe. Mkuu wa Wilaya pia amewaasa wazazi wote ifikapo tarehe 8 January, 2023 watoto wote waliofaulu wawe wameripoti shuleni.
Pia amewaasa wananchi kuelekea msimu wa Sikukuu za Chirsmas na mwaka mpya kuwa makini hasa katika suala zima la ULINZI na usalama. washerehekee kwa Amani waachane na ulevi wa kupindukia pamoja na ugomvi.
Mhe Kahabi kipekee amewapongeza wananchi wa Rusumo kwenye Suala zima la usafi Kwa wananchi kushirikiana na viongozi kufanya usafi wa Mazingira katika Kata hiyo ya Rusumo.
Mhe Kanali Mathias J.Kahabi mkuu wa Wilaya aliyesimama kulia akiwa na Ndg Solomon O.Kimilike wa kwanza kushoto.wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara kusikiliza na kutatua kero za Wananchi kata ya Rusumo Wilayani Ngara.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza na kutatua kero kata ya Rusumo.
Mhe Mkuu wa Wilaya aliyesimama akiongea na Wananchi wa Rusumo Wilayani Ngara katika zoezi la Oparesheni Tatua kero za Wananchi.
Kamati ya Usalama na wataalam waliokaa wakiwa katika Mkutano wa Hadhara Oparesheni Tatua kero.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa