- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakulima wa mibuni katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kupanda miche ya kisasa ya zao hilo, ili waweze kuongeza uzalishaji kwani miche ya zamani haina tija tena kwa wakulima hao.
Hayo ni kwa mujibu wa Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Constantine Mudende, alipokuwa akiongelea umuhimu wa kupanda miche ya kisasa ya mibuni ofisini kwake Oktoba 18, 2018.
“Miche ya zamani ipuruniwe na kama inawezekana ing’olewe kabisa, ipandwe miche ya kisasa ambayo inatoa mazao mengi, ili iweze kuongeza kipato cha wakulima wa zao hili na kuwaondolea umasikini.” alisema Ndugu Mudende.
Amesema baadhi ya wakulima wana miche yenyeumri wa miaka zaidi ya 80, ambapo uzalishaji wake hauna tija tena kwa wakulima, na kuongeza kwamba miche ya kisasa itawaongezea kipato na hivi kuwainua kiuchumi.
Aidha, amesema katika msimu huu; Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers Cooperative Limited, kimefanikiwa kukusanya zaidi ya tani 980 za kahawa aina ya Arabika, ambapo zaidi ya shilingi bilinioni 1.2 zimetumika kununulia kahawa hiyo.
Kwa kununua kiasi hicho cha kahawa ya Arabika, alisema ndugu Mudeded, wamefanikiwa kuvuka lengo la kununua tani 500 msimu wa 2017/2018, huku akidai kwamba wamevuka lengo ya serikali kuagiza kahawa yote, ikusanywe na vyama vya ushirika.
Ameongeza kwamba kabla ya agizo la serikali; kahawa nyingi ilikuwa ikivushwa kwenda nchi jirani, lakini msimu huu wakulima wamedhibitiwa, kwa hiyo wanatarajia kukusanya zaidi ya tani 2500 za Robusta msimu huu.
Mwanzoni walilenga kukusanya tani 1500 za Robusta, lakini dalili zinaonesha kwamba wanaweza kukusanya zaidi, kwani wakulima bado wana kahawa nyingi majumbani kwao, na bado wanaedelea kuvuna.
“Benki ya Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) imetukopesha shilingi milioni 700, kwa ajili ya kununua kahawa ya Robusta, fedha hiyo ni kidogo kwa kahawa tunayotarajia kukusanya, lakini tunatarajia kuuza kahawa ya Arabika, hivyo itatuongezea mtaji wetu.” alisema Ndugu Mudende.
Ndugu Mudende ameishukuru benki ya TADB, kwa kuwapatia mkopo wa shilingi za kitanzania billion mbili, ambazo zimetumika kununulia kahawa ya aina ya Arabika na wanaanza kununua kahawa aina ya Robusta.
Akiongelea ikiwa chama cha Ushirika kitakuwa na uwezo wa kulipa deni hilo; amesema bila shaka yoyote, chama hicho kitalipa deni hilo, ingawa inaenekana bei ya kahawa mnadani kuwa chini, bado chama hicho kina uwezo wa kulipa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa