- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Imefanyika hafla ya ugawaji mipira kwa Halmashauri 8 za Mkoa wa kagera, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa kagera.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi wa chama Cha mpira wa miguu Mkoa wa kagera (KRFA) wakiongozwa na Mkiti Ndg. Salum Umande Chama, Viongozi wa vyama vingine vya Mkoa.
Maafisa Elimu Msingi Halmashauri zote za Mkoa, Maafisa michezo/utamaduni Wilaya zote, walimu wa Michezo Manspaa na wanafunzi wanamichezo kutoka Manspaa ya Bukoba.
Mgeni Rasmi katika hafla ya kukabidhi mipira ya soka alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa kagera Mhe Hajatt Fatma Abubakari Mwassa aliyewakilishwa na Mkuu Wa Wilaya ya Bukoba Mhe Erasto Sima.
Taarifa iliwasilishwa na Afisa Michezo Mkoa wa kagera Ndg Kepha Elias Kepha ambaye aliwashukuru Shirikisho la mpira wa miguu- TFF pia Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa hamasa Kubwa katika michezo Kwa Kutoa fedha Kwa Kila goli michezo ya kitaifa.
Nae Mkiti wa Chama Cha mpira wa miguu Mkoa wa kagera KRFA Ndg. Salum Chama alisema lengo kubwa la Kutoa mipira hiyo ni kuibua vipaji vya soka toka shule za Msingi.
Mgeni Rasmi Mhe Sima alisema mipira hiyo ikawe chachu ya kukuza taalum shuleni, somo la michezo lifundishwe Kwa wanafunzi kwa Vitendo,shule ziwe na hati Miliki vikiwemo viwanja vya michezo , wanafunnzi aendelee kufundishwa uzarendo ikiwa ni pamoja na nyimbo ya Afrika Mashariki.
Pia Halmashauri zitenge Fedha Kwa ajili ya Kitengo Cha michezo Sanaa na utamaduni Kwa ajili ya mafunzo ya michezo.
Mhe Sima alisisitiza tupende michezo na pia kuipenda timu yetu inayowajiliaha Mkoa wa kagera (Kagera sugar) aidha maafisa michezo wawe wanafika kwenye michezo ya Kagera sugar inapocheza,, aliendelea Kwa kusema michezo ni sehemu ya Maisha.
Mwisho Mhe Sima Alimpongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ni mwanamichezo namba moja na kuwapongeza Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kwa Kutoa mipira Kwa ajili ya kukuza na kuibua Vipaji vya michezo shuleni.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe Erasto Sima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa kagera Mhe Hajatt Fatma A. Mwassa katika hafla ya ugawaji Mipira ya soka Kwa Halmashauri 8 za Mkoa wa kagera iliyofanyika Ukumbi wa mkuu wa mkoa.
Mhe Sima akikabidhi Mipira 100 Kwa kaimu Afisa Elimu Msingi Ndg Ezekiel Zabayanga na Afisa Michezo / Utamaduni Ndg said Salum katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Mhe Erasto Sima Mkuu wa wilaya Bukoba akiwa na Afisa Michezo Mkoa wa kagera Ndg. Kepha Elias Wakikabidhi mipira Kwa Afisa michezo na utamaduni Ndg. Swirtbert Mujemula Halmashauri ya Bukoba katika hafla ya ugawaji mipira iliyofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa kagera.
Maafisa Michezo wakiwa kwenye hafla ya ugawaji Mipira Kwa Halmashauri 8 za Mkoa wa kagera.
Wanafunzi wanamichezo Kutoka manspaa ya Bukoba wakiwa kwenye picha Pamoja na Mhe Erasto Sima Mkuu wa wilaya ya Bukoba , Ndg kepha Elias Afisa michezo Mkoa kagera , Ndg Salum Umande Chama Mkiti KRFA, na Mwl Ezekiel Zabayanga kaimu Afisa Elimu Toka Ngara na Mwl. Marwa afisa elimu Msingi toka kyerwa.
Mhe Sima akikabidhi Mipira kwa Afisa michezo Ndg Denis toka Muleba.
Afisa michezo Misenyi akipokea Mipira Kutoka Kwa mkuu wa wilaya Mhe Erasto Sima.
Afisa Elimu Msingi karagwe akiwa na Afisa michezo wa karagwe wakipokea Mipira kutoka Kwa Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe Erasto Sima.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa