- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila leo tarehe 21.01.2023 ametoa maelekezo kwa viongozi wa ngazi zote za Wilaya kuanzia Wakuu wa Wilaya kushirikiana na Halmashauri, Tarafa, Kata na Vijiji kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kabla ya tarehe 31.01.2023 na kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wawe wameripoti na kuanza masomo.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika eneo la ofisi yake, ameeleza kuwa mzazi yoyote atakayebainika kutorosha mtoto au kufanya vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Pia kuanzia sasa, Wakuu wa Wilaya wapokea taarifa ya kila siku kutoka kwa Wakuu wa shule ili kuona changamoto ni nini inayopelekea wanafunzi hao wasiripoti shuleni hadi sasa.
"Kwa Mkoa wa Kagera, wanafunzi waliochagulia kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 59,324 ambapo tulitarajia wawe wameripoti wote, hadi kufikia jana tarehe 20.01.2023 wanafunzi 35,594 sawa na asilimia 60 ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza wameripoti shuleni hivyo wanafunzi 23,730 sawa na asilimia 40 bado hawajaripoti kwenye shule walizochaguliwa", ameeleza Mhe. Chalamila
Ameendelea kueleza kuwa Mkuu wa Shule yoyote atakayebainika anawakwaza wazazi kwa kuanzisha michango ambayo haipo katika utaratibu na kuweka msimamo wa kutokupokea wanafunzi kwasababu hana mchango watachukuliwa hatua za kinidhamu. Na kuwataadharisha wazazi waliowaficha watoto wao kwa maana ya kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya kisheria hii italeta nidhamu kwa mujibu wa Sera ya Elimu kuwa elimu hii ni ya lazima kwa mwanafunzi yoyote anayechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Ameongeza kuwa kila shule iwashirikishe wazazi na kuhakikisha kuwa inatoa chakula cha mchana kama ilivyotamkwa katika waraka namba 3 wa Elimu wa Mwaka 2016 ili iwe kivutio kwa wanafunzi kubaki shule na kusoma wakiwa na utulivu hawana njaa hivyo chakula kwa wanafunzi si mchango bali ni hitaji la msingi kama ilivyo mavazi na kama ilivyo nyakati za usingizi kuhitaji kulala.
Aidha, ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais amewekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya madarasa pamoja na miundombinu mingine kama Maabara, matundu ya vyoo pamoja na nyumba za walimu. Pamoja na uwekezaji huo uliofanywa kwa Mkoa wa Kagera awamu ya kwanza madarasa 881 na awamu ya pili madarasa 514 ilitarajiwa kuwa kiwango cha wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kiongezeke kutokana na hamasa hiyo na wanafunzi waripoti kwa wakati.
Jambo lingine alilolifanya Mheshimiwa Rais ni kuendeleza Sera ya Elimu bure kuanzia awali mpaka kidato cha sita. Kwa mantiki hiyo ilitarajiwa inapofika mwezi Januari mwaka huu wa 2023 wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza waripoti haraka shuleni kwasababu hakuna mkwamo wa madarasa na ada kama ilivyokuwa hapo awali. Hivyo kuhakikisha madarasa yaliyojengwa na Mheshimiwa Rais wanafunzi wanaripoti shuleni na wanaendelea kusoma kama ambavyo yeye amekusudia zaidi kuendeleza uwekezaji wa madarasa na ajira za walimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa ni bora kwa kikazi cha sasa na vijavyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa