- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara anawatakia wananchi wote wa Wilaya ya Ngara HERI YA SIKUKUU YA MWAKA MPYA 2024
Mhe Mkuu wa wilaya amesema: "Ninawaomba wananchi wote kusherehekea Sikukuu hii ya Mwaka Mpya kwa Amani na Utulivu na kujiepusha kwa namna yeyote ile na Uvunjifu wa Amani kabla, wakati na baada ya Sikukuu hizo"
Aidha,aliendelea Kwa kusema Mhe Mkuu wa wilaya "Nawaasa wazazi wote ambao watoto wao wameandikishwa kujiunga na darasa la kwanza na wale ambao wamechaguliwa kujiunga na Secondary Kidato cha Kwanza kuhakikisha watoto hao wanaripoti Shule January 2024 kwa muda uliopangwa bila kukosa kwa kisingizio chochote kile."
Pia, "wakati wa Sherehe hizi ni marufuku Wamiliki wa Kumbi za Starehe kupiga Disco maarufu kama Disco Toto Atakayekiuka maagizo haya hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yake" amesema Mhe Mkuu wa Wilaya.
Pamoja na maagizo hayo, Mhe Mkuu wa Wilaya Col Mathias Julius Kahabi amesema Vyombo vya Usalama Wilayani Ngara vimejipanga vema kufanya doria za mara kwa mara kila sehemu ili kuhakikisha Wananchi wanamaliza sherehe hizi kwa Amani na Utulivu wa Kutosha. Rai yangu Wananchi hususani wazazi ambao watoto wao wanatakiwa kwenda shule Mwakani kufanya Sherehe za kiasi huku wakiweka akiba ya hela kwa ajili ya kupeleka watoto wao shule ifikapo January 2024. Nawatakia Maandalizi mema ya Sikukuu ya Mwaka Mpya 2024 na Mungu awabariki sana. Wenu katika kuwatumikia
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa