- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ndugu wananchi, Mimi Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wa wilaya ya Ngara naomba kuleta salamu za shukurani kwenu, Tarehe 12 Agost, 2023 tulianza shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa uhuru kiwilaya, tumekuwa pamoja tangu siku ya Jumamosi tumekesha uwanja wa Posta, na tumekesha Stendi Benaco Jumapili Tar 13-8-2023
Ndugu wananchi, Tarehe 14 Agost, 2023 tumeupokea mwenge wa uhuru wilaya ya Ngara pale stendi ya Benaco - Kasulo, ikumbukwe kwamba Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhika na miradi yote na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi yote wilayani Ngara yenye thamani ya Tsh 1,756,917,663.93.
Kwa heshima kubwa naomba kuwashukuru wananchi na VIONGOZI wote wa Ngara kwa ushirikiano na Mshikamano mkubwa mliouonesha muda wote wa Shughuli za Mwenge wa Uhuru Wilayani Ngara toka mapokezi yake tarehe 14/8/2023 pale Benaco hadi Makabidhiano pale Nyakahura - Wilaya ya Biharamulo tarehe 15/8/2023, Mwaka huu umekua wakipekee sana Ngara Kimapokezi.
Ndugu wananchi, watumishi na wasio watumishi wa serikali, Wafugaji na wakulima, WAKIMBIZA MWENGE KIWILAYA, waandishi wa habari kutoka Wasafi Tv, Star Tv, ITV, Redio Kwizera, Ngara Tv, Bilomo Tv, Dedu Production, Dulla Uwezo Media, Number one Production, Kasibante FM na Media zote kipekee naomba kusema Ahsanteni sana na ninawaomba muendelee na moyo huo na Mungu azidi kuwabariki katika kazi zenu za kila siku.
IMETOLEWA COL. MATHIAS JULIUS KAHABI MKUU WA WILAYA YA NGARA
16 AGOST, 2023
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa