- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce, ametembelea vyuo vya Mafunzo ya Ufundi standi (VETA), ili kuona ajionee maendeleo ya ujenzi wa vyuo hivyo, ili viweze kuwasajili vijana waliohitimu elimu ya msingi na kidato cha nne.
Prof. Ndalichako amefanya ziara Januari 26, 2019 mkoani Kagera, ambapo alipata fursa ya kutemebelea eneo litakalojengwa chuo kikuu cha ufundi kijijini Burugo, kujionea kama serikali ya Mkoa wa Kagera imefikisha miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme katika eneo hilo.
Akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro alikagua miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme iliyofikishwa katika eneo hilo na Serikali na kusema kuwa jukumu la Serikali, limekamilika; kilichobaki ni Watu wa China kuanza ujenzi wa chuo hicho.
“Sisi tumekamilisha kilichotakiwa, kilichobaki ni Serikali ya Watu wa China kuanza ujenzi katika eneo hili, chuo hiki kikamilika kitapokea wanafunzi 800 wa fani mbalimbali kwa wakati mmoja, na kitagharimu Shilingi bilioni 22.4.” Alifafanua Profesa Ndalichako.
Serikali ya Watu wa China mwaka 2015, ilihaidi kutoa shilingi bilioni 22.4 kwa ajili ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi, na Rais Jakaya Kikwete akaagiza chuo hicho kijengwe Mkoani Kagera, sasa ujenzi huo, unatarajia kuanza Mei 2019; baada ya taratibu kukamilika.
Profesa Ndalichako ametembelea ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Wilayani Karagwe (Karagwe Development Vocational Training Center KDVTC), ambapo Serikali ilitoa Shilingi bilioni 4.6 ili Chuo hicho kiboreshwe miundombinu, ili kiweze kupokea wanafunzi wengi zaidi.
Profesa Ndalichako amemwagiza Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoani Kagera Mhandisi Salum Chanzi, ahakikishe ujenzi unakamilika ifikapo Julai 2019 kama ilivyopangwa wakati uataratibu wa ukarabati wa chuo hicho.
Aidha, katika hatua nyingine Profesa Ndalichako ametembelea Shule ya Sekondari Bukoba na kukagua majengo yaliyoezuliwa na upepo Octoba 17, 2018, na kuathiriwa na tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016 na kuhaidi kutoa fedha ili shule hiyo, ikamilike wananafunzi waendelee na masomo katika Shule hiyo.
Mara baada kupokea taarifa ya mkoa ya maendeleo ya elimu Mkoani Kagera, aliupongeza uongozi kwa kufanya vizuri na kuwa katika nafasi za kumi bora, katika mitihani ya taifa, huku akiagiza utatuzi wa changamoto za miundombinu.
“Chanagamoto ya vyoo inatakiwa kufanyiwa kazi haraka ukizingatia kuwa mkoa huu, una mvua nyingi, jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha ya watoto wawapo shuleni.” Alisisitiza Profesa Ndalichako.
Mkoa wa Kagera unafanya vizuri katika matokeo mbalimbali, na kuwa miongoni mwa mikoa kumi bora, ambapo kwa miaka mitatu mfurulizo 2016, 2017, na 2018 Mkoa wa Kagera uliongoza kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara katika Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne.
Pamoja na Mkoa wa Kagera kufanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018, shule ya Sekondari Rwemondo Wilayani Missenyi, ilishika nafasi ya 4 kwa shule kumi za mwisho.
Na Sylvester Raphael
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa