- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imesitisha vyama vya ushirika vya Kagera Development Cooperative Union (KDCU) LTD cha wilaya za Karagwe na Kyerwa, Kagera Cooperative Union (KCU) na Ngara Farmers mkoani Kagera kulipa madeni hadi Wizara ya Kilimo itakapotoa maelekezo na utaratibu mwingine.
Hayo ni kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Innocent Luga Bashungwa, wakati akiongea na vyombo vya habari mkoani Kagera, alipokuwa akitoa mrejesho wa hatua zinazochukuliwa na wizara hiyo kuhusu wakulima wa kahawa watakavyo nufaika na zao hilo.
Mhe.Bashungwa ametaja moja ya sababu za kusitisha madeni hayo kuwa vyama vya ushirika kutumia mapato yanayopatikana kulipa madeni badala ya kuwalipa wakulima, ambao amewataja kuwa ndo wenye mali.
Wakati huo huo, Chama cha Ushirika cha Farmers Corporative katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kilikadiria kununua tani 500 za kahawa aina ya Alabaika, lakini kimenunua zaidi ya tani 900, katika msimu wa 2017/2018.
Meneja wa Ngara Farmers Corporative Ndugu Amphrey Katakweba amesema mwanzoni walifanya maksio ya chini, hivyo walipata fedha kidogo za kukusanyia kahawa hiyo, ikilinganishwa na hali halisi ya kahawa ya Alabika, waliyozalisha wakulima katika msimu wa huu.
Amekiri kuwa kahawa ya mkoa wa Kagera hasa ile ya wilayani Ngara, ina ubora mzuri sana, huku akiomba msaada wa kupata sehemu ya kutunzia kahawa iliyokwisha kusanywa; na kuongeza kwamba chama cha ushirika kimepoteza mapato, kwa kushindwa kukusanya kahawa katika kipindi cha miaka minane iliyopita.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa