- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .Imetoa fedha Tsh Bilion 1,163,800,000/kupitia mradi wa Boost Kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya , Vyumba vya Madarasa kwa shule za Msingi 8 pamoja na ujenzi wa Matundu ya Vyoo.
Shule zilizopatiwa vyumba vya Madarasa ni Bugarama Vyumba 2, Kabanga Vyumba 4 na Matundu ya Vyoo 3, Kanyinya Vyumba 5 na Matundu ya Vyoo 3, Kumuyange Vyumba 6 na matundu ya Vyoo 3, Muyenzi Vyumba 5 na Matundu 4, Keza Vyumba 4 na Matundu ya Vyoo 6 ,Njiapanda Vyumba 4 na Matundu ya Vyoo 3 pia Shule Mpya Kumunazi Vyumba 7.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon Kimilike alimshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuonyesha upendo wake mkubwa Kwa wananchi wa Ngara kuendelea kuleta fedha za Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Ngara.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Wilaya alisema atahakikisha fedha hizo zinasimiwa vizuri Kwa kuhakikisha miundombinu ya madarasa na vyoo vinajengwa Kwa ubora.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa