- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeleta fedha mwezi January 2024 Tsh 1,816,000,000.00 na Tsh 1,326,600,000.00/= Jumla Tshs Billion 3,742,600,000.00/= Kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Wilaya Ngara.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon O. Kimilike fedha hizo Kwa ajili ya Miradi ya Afya 4, Elimu Msingi ujenzi wa matunda vyoo 13, Ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 na Bweni la wanafunzi Wenye mahitaji Maalum shule ya Msingi Murgwanza, Kwa Elimu Sekondari ujenzi wa vyumba vya madarasa 26, ujenzi wa matundu ya vyoo 30 ( high school), ujenzi wa vyumba vya madarasa 45 mapya kidato Cha kwanza na matundu 96 ya vyoo kidato Cha kwanza 2024.
Aidha Mkurugenzi wa wilaya Ndg Solomon O Kimilike amemshukuru na kumpongeza sana Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa Juhudi anazozifanya za kuwaletea Maendeleo wananchi wa Wilaya ya Ngara kwa kuleta fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo Afya, Elimu Msingi, sekondari , Maji na Barabara.
Mkurugenzi Solomon alimalizia Kwa kuwashukuru Mhe Mkuu wa Wilaya Kanali Mathias J Kahabi Kwa ushirikiano wake mkubwa katika usimamizi na ufuatiliaji Miradi yote ya Maendeleo Wilayani pia Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G.Ruhoro Kwa ufuatiliaji wake wa fedha za Miradi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa