- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Wilaya ya Ngara leo imehitimisha maadhimisho ya miaka 60 ya muungano katika viwanja vya Posta ya zamani na kumalizika katika ukumbi wa community centre na ndipo hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ilipooneshwa kwa wananchi wote waliohudhuria tamasha hilo.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe. Col Mathias Julius Kahabi ndie aliekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Mhe Mkuu wa Wilaya pamoja na wananchi walikagua na kuona baadhi ya vikundi vya ngoma za asili Pamoja na kuangalia maonesho ya vyakula vya asili, michezo pamoja na vikundi vya burudani.
Pamoja na hayo mdahalo uliendelea katika maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Lakini pia Mkuu wa wilaya alihotubia hadhara hiyo katika maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano yamefanyika tarehe 25/4/2025 yakipambwa na Maonesho ya vitu vya asili, kama vyakula vya asili, burudani, michezo na mengine mengi.
Mhe. Mkuu wa Wilaya na mgeni rasmi wa maadhimisho haya akikagua maonesho ya vitu vya asili ya Ngara.
Vikundi vya Ngoma kwenye maonesho ya vitu vya asili.
Jinsi walivyokuwa wakisaga nafaka zamani kwa sababu hapakuwepo na mashine za kusaga.
Baba Askofu Ruzige akiliombea Taifa Na Viongozi.
Hotuba ya mgeni rasmi Mhe. mkuu wa Wilaya ya Ngara col. Mathias Julius Kahabi kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa