- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi wilayani Ngara ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ngara mh. Alex Gashaza akihutubia mbele ya jopo la wafanyakazi waliojitokeza kusherehekea sherehe hizo katika viwanja vya posta wilayani Ngara. Katika mambo ya msingi aliyoyagusia ni kuwaasa watumishi wote kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha serikali kufikia malengo yake lakini piakuwa na kauli nzuri kwa wale wanaowatumikia. Alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya "HAPA KAZI TUU!" hivyo ni vyema kila mtu akawajibika kwa nafasi yake. Aliongeza kuwa ana uhakika kuwa serikali ina mipango mizuri ya kuboresha maisha ya watumishi kwa kujali maslahi yao. Alishauri maneno ya vijiweni na watu wachache yasiwakatishe tamaa watumishi bali waendelee kuchapa kazi. Sherehe hizo ziliambatana na utoaji wa vyeti kwa wafanyakazi bora wa mwaka 2016/2017.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa