- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kunyunyizia dawa ya kuua mbu majumbani, ili waweze kuutokomeza ugonjwa wa Malaria ifikapo Mwaka 2022.
Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jenel. Marco Elisha Gaguti, alipofanya ziara ya siku moja Oktoba 29, 2918 katika Wilaya ya Ngara, ili kujionea mwenyewe zoezi la kunyunyizia dawa ya ukoko linavyoendelea wilayani humo.
“Nimefika kata ya Rusumo katika kijiji cha Mshikamano, na kufanya tathimini ya zoezi la kunyunyizia ukoko majumbani linavyoendelea, nimeona linaendelea vizuri, kwa maana kwamba wanaofanyakazi hiyo, wamepata ushirikiano wa kutosha ingawa siyo kwa 100%”. Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Amesema lengo la serikali ni kwamba zoezi hili lifikie 100%; huku akiwataka viongozi wa vijiji na kata, kuwahamasisha wananchi kujitokza kwa wingi, ili zoezi lifanikiwe na hatimaye Malaria iwe Historia katika mkoa wa Kagera na taifa kwa ujumla.
Kutokomeza Malaria hapa nchini kunawezekana kwani uzoefu unanesha kwamba mkoa wa Kagera mwaka 2015/2016, ulikuwa na asilimia 42% za maambukizi, lakini takwimu za mwaka 2017/2018 zinaonesha kwamba mkoa umekuwa na maambukizi kwa 15.1%.
Hata hivyo, amesema amemua kufanya ziara katika wilaya ya Ngara, na wilaya nyingine zoezi hili linapoendelea, ili aweze kujionea mwenyewe linavyoendelea na kama kuna changamoto, aweze kuitafutia ufumbuzi kama mkoa.
Amesema changamoto aliyoiona ni upungufu wa vingozi wa kuowaongoza, na kuwahamasisha wananchi, waweze kujitokeza na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wanaopiga dawa, hivyo akaahidi kushirikiana na viongozi wengine ngazi ya mkoa kuhakikisha changamoto hiyo inaondoka.
Aidha, amesema kwamba viongozi wate wamepewa dhamana, hivyo ni vema wakawajibika katika hili, ili wahakikisha wananchi wote wanashiki kikamilifu katika zoezi hili, ili malengo ya serikali yaweze kutimia.
wakati huo huo, Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Dr. Revocatus Ndyekobora, amewataka viongozi wa vijiji, vitongoji na wa kata watoe ushirikiano katika kuhakikisha kwamba wananchi wote wanashiki kikamilifu katika zoezi hili.
Amesema wahamasishaji walioteuliwa na wilaya ni wa chahche kuweza kuwapitia wananchi wote, hivyo, akawataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha zoezi hilo, huku akisisitiza kwamba zoezi hili ni la kitaifa, hivyo lazima wahakikishe linafanikiwa.
“Malaria ni ugonjwa mbaya hasa kwa aja wazito na watoto chini ya miaka mitano, kwa hiyo tuendelee kutoa ushirikiano kwa jitiada zinazofanywa na serikali, ili tuutokomeze kabisa”. Alisema Dr. Ndyekobora.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa