- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imeipatia Halmashauri ya wilaya ya Ngara, jumla ya vitabu 4,916 kati ya 9,832 vya mitaala mipya vinavyotarajiwa kuletwa, kwa ajili ya kujifunza na kufundisha watoto wa darasa la nne.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amesema kwamba hizo ni juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Amesema aerikali itaendelea kuziwezesha shule za sekondari na za msingi kwa kutoa vitendea kazi, kadiri rasilimali ya kugharimia vifaa hivyo itakavyokuwa inapatikana.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Ngara, amesema kwamba idadi ya watoto inaongezeka kila mwaka, na kwamba ongezeko hilo haliendi sambamba na ongezeko la vifaa vinavyohitajika, kwa ajili ya kufundishia watoto wao.
“Tunaishukuru serikali kwani katika kutimiza lengo la kuboresha elimu hapa nchi, tumepokea shilingi milioni 142, kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, na shilingi milioni 152, kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi.” Alisema mkuu huyo wa Wilaya Lt. Col. Mntenjele.
Aidha, amesema wazazi wanawajibika kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo yao, na wanasoma kikamilifu, huku wakifuata maelekezo ya walimu, ili kufanikisha lengo la taifa la kutoa elimu bora kwa wanafunzi na si bora elimu.
Amekemea tabia ya wazazi kuwazuia watoto kuhudhuria shule, ili washiriki shughuli za kilimo, kuchunga mifugo pamoja na shughuli nyinigine zisizohusu masomo, zinawazuia watoto hao kupata haki yao ya msingi ambayo ni elimu.
Naye Afisaelimu Idara ya Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Mwesiga, amesema kwamba idara yake imefanikiwa kuwasajili watoto wa kujiunga darasa la kwanza, na la awali kwa zaidi ya 100%.
Anaishukuru serikali kwa kuiwezesha idara yake kupata vitabu vya darasa la nne vya mitaala mipya, kupata fedha za kujenga madarasa, pamoja na vifaa vingine muhimu vinavyosaidia shughuli za kufundishia na kujifunzia.
Hata hivyo amesema kwamba pamoja na mafanikio hayo, idara yake ina matatizo ya upungufu wa nyumba za walimu, wazazi kuwashawishi watoto kufanya vibaya mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba, pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa