- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kutoa kipaumbele katika elimu kwa kuwasaidia vijana waliomaliza kidato cha nne waweze kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano.
Wito huo umetolewa na Kaimu Afisaelimu idara ya sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Marton James Juni 26, 2018 kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Ndugu Marton amewaambia wadau elimu kwamba shule ya sekondari ya Rusumo inatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha tano chaguo la pili mwaka wa masomo 2018/2019, lakini kwa sharti kwamba miundombinu kadhaa ikamilike.
Amesema kwamba wakaguzi wameridhika na hali ya shule ilivyo na kushauri baadhi miundombinu ifuatayo ikamilike kabla ya shule hiyo; ameitaja kuwa ni kuongeza matundu matano ya vyoo 5 kwa ajili ya wasichana.
Miundombinu mingine ni kujenga eneo la haja ndogo na matundu mawili ya vyoo kwa ajili ya wavulana, kujenga mabafu vyumba 5 kwa ajili ya wasichana na wavulana, kujenga shimo la kudumu la taka, pamoja na kujenga jiko la kudumu.
Nao wadau wa elimu wamelipokea wazo hilo na kuahidi kuchangia gharama za kukamilisha miundo mbinu hiyo ambapo baadhi yao wameahidi kutoa mabati, simeneti pamoja na tripu za mchanga na mawe.
Shule ya sekondari ya Rusumo itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano chaguo la pili katika mwaka wa masomo wa 2018/2019, ikiwa miundombinu hiyo itakamilika kwa wakati.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa