- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti, ameutaka uongozi wa Wilaya ya Ngara, kuwa na msimamo thabiti, uandilifu na umakini katika kusimamia mradi wa Local Area Development Plan (LADP) ili uwe na tija kwa walengwa.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera ameyasema hayo Novemba 26, 2018, ofisini kwake wakati akiongea na wakuu wa Wilaya ya Ngara, waliofanya ziara ya siku moja ofisini kwake, kwa lengo la kumfafanulia malengo na faida za mradi huo kwa wananchi.
“Ninavyoona sasa Ngara inakwenda kubadirika itakuwa mpya, kinachotakiwa ninyi kama viongozi, ni kuwa na msimamo na usimamizi thabiti, ili malengo mazuri ya mradi huo yatimie.” Alisema Brig. Jen. Gaguti.
Amesema miradi hiyo imekuja wakati muafaka, kwani wilaya inakabiriwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoingia awali, darasa la kwanza na kidoto cha kwanza mwakani.
Amesema mradi huo ni mkubwa kwani kukamilika kwa vituo vya afya vya Rusumo na Lukole kutasaidia kwa kiwango kikubwa huduma za afya kwa wananchi wa Halmashauri ya Wikaya ya Ngara.
Ameahidi kutembelea mradi huo pindi itakapoanza, ili aweze kujionea mwenyewe; huku akiwasisitiza viongozi wa wilaya ya Ngara, kuwahamasisha wananchi wajitolee katika kufanikisha mradi huo, ili fedha hiyo iweze kuwa na tija zaidi.
Amewashauri kuwa wavumilivu na wastahimilivu kwa madai kwamba matatizo na changamoto, lazima ziwepo katika kutekeleza mradi mkubwa namna hiyo, kwani walipo watu lazima changamoto ziwepo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele ameahidi kuhakikisha mradi huo, unatekelezwa jinsi ulivyopangwa na walengwa wananufaika na mradi huo; tayari watanzania kadhaa wameajirawa katika mradi huo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema wananchi wanaoathirika na mradi huo, wanalalamika kwamba wao hawapati ajira bali watu kutoka mbali ndio wanaoajiriwa, wanasahau kwamba ajira zinatolewa kwa elimu kwa kiwango cha elimu.
Amekiambia kikao hicho kwamba wakati wa kupasua miamba baadhi ya nyumba za wananchi zilipata nyufa, lakini baadhi ya wananchi hao wanagoma kupokea fidia hiyo kwa madai kwamba fedha ni kidogo.
“Watu hawataki kufidiwa kulingana na madhara yaliyotokea, wanataka wapewe fedha zote, kasha tuwahamishe wakajenge sehemu nyingine; wanaomba hivyo, kwa sababu watu waliolipwa fidia kutoka Benki ya Dunia walipata fedha nyingi.” Alisema Lt. Col. Mntenjele.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa