- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G Ruhoro ametoa tairi za pikipiki zenye thamani ya TZS 2,000,000.00 kwa waratibu wa Elimu kata zote 22 za Wilaya ya Ngara.
Lengo la kutoa tairi hizo ni kuwawezesha kuweka tairi mpya kwenye pikipiki zao ili waweze kuzunguka kata zao kuhamasisha Elimu ili kuendelea kukuza na kuinua viwango vya taalumu Wilayani Ngara katika serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania MAMA DR SAMIA SULUHU HASSAN.
Lengo la Mh Ruhoro ni kuwezesha kufanikisha ndoto za wazazi wengi wa Ngara zinazolenga kuona watoto wao wakifaulu na kuendelea na masomo ngazi za Elimu zinazofuata . Kwa majitoleo haya, uratibu na usimamizi utaendelea kuimarika na hivyo kuwafanya watoto wa wana Ngara kufaulu vizuri kwenye mitihani yao ya Elimu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa