- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
TAARIFA YA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA WILAYA YA NGARA MKOA WA KAGERA KUANZIA JANUARI 2024 – 25/04/2024
1:0 UTANGULIZI.
Wilaya ya Ngara ilianza maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu Mwezi Januari 2024 – 25/04/2024 kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo ni upambaji wa Ofisi za Serikali na Uwekaji wa picha za Viongozi, usafi wa mazingira, upandaji miti, uandishi wa Insha, michezo sanaa na utmaduni, maombi ya Dua kuliombea Taifa, Tamasha la usiku wa Muungano, burudani na vyakula mbalimbali, kutazama hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupiga fataki.
2: ITIFAKI.
Itifaki ilizingatiwa wakati wa shughuli mbalimbali za Maadhimisho ya miaka 60 Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Mwongozo.
2:1 UPAMBAJI WA OFISI ZA SERIKALI.
Zoezi la upambaji Ofisi za Serikali na Taasisi binafsi lilifanyika kwa kuweka mapambo ya Bendera ya Taifa, picha za Viongozi Waasisi wa Muungano Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ally Mwinyi. Kuliwekwa pia vitabu vya Kusaini eneo la mapambo. Maeneo yaliyopambwa ni pamoja na Ofisi za Mhe: Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Taasisi za Umma kama benki, Ofisi za Serikali Kuu TARURA, TANESCO, NGUWASA, TRA na Chuo cha Ufundi Remela. Meneo mngine ni pamoja na shule za Umma na binafsi na Taasisi binafsi. Viongozi na Wananchi wanaendelea na zoezi la kuenzi Muungano wetu kwa kusaini hadi Tarehe 03/05/2024. Aidha jumla ya wananchi 160 walisaini vitabu vya maadhimisho ya Muungano katika Ofisi za Mhe Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
3:0 UPANDAJI WA MITI
Jumla ya miti 2500 ilipandwa katika shule ya sekondari ya wavulana ngara (ngara high school) na viongozi mbalimbali wakiongozwa na mhe. mkuu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanzania. Aidha jumla ya miti 34,500 imepandwa na viongozi na wananchi kuanzia mwezi januari 2024 hadi tarehe 23.04.204. Miti hiyo imepandwa katika Kata zote za Wilaya ya Ngara pamoja na Taasisi mbalimbali za Umma.
4:0 USAFI WA MAZINGIRA.
Zoezi la Usafi wa mazingira lilifanyika kwa Viongozi na Wananchi kufanya usafi maeneo yoe ya Wilaya hususani Makao Makuu ya Kata na kwenye Vijiji.
5.0 MICHEZO, SANAA NA UTAMADUNI
Katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano shughuli mbali mbali za michezo, Sanaa na Utamaduni zilifanyika katika Wilaya ya Ngara kama ifuatavyo:
5.1: MICHEZO
Michezo iliyofanyika ni pamoja na mpira wa miguu kati ya shule ya sekondari Mumiterama na shule ya sekondari Ngara. Katika mchezo huo Mumiterama ilipata ushindi wa goli moja. Katika mchezo wa Netiboli zilishindana Mabawe sekondari na timu ya Watumishi (Ngara Queens) ambapo timu ya Watumishi ilishinda kwa magoli 7 kwa 5.
5.2 UTAMADUNI
Katika kipengele hiki zilifanyika ngoma za asili, nyimbo na maonesho ya vyakula na vitu vya asili. vikundi vilivyoshiriki ni Umoja Group, Kina Mama Nyamiaga, Kina Mama Mubinyange, Upendo Group na Shirikisho la Wasanii.
5:3 UANDISHI WA INSHA.
Zoezi la uandishi wa Insha lilifanyika kwa Shule za Msingi na Shule za Sekondari kwa kuwashindanisha ili kupata waandishi washindi mahili. kwa Shule za Msingi washiriki wawili (8) waliandika insha na Shule za Sekondari washiriki watano (19). Insha ziliwasilishwa Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari ili kupata washindi 3 kila Idara ambapo walizawadiwa fedha taslimu Tsh. 30,000 mshindi wa kwanza, Tsh 20,000.00 mshindi wa pli na Tsh. 10,000.00 kwa mshindi wa tatu.
6.0 TAMASHA LA USIKU WA MUUNGANO
Tamasha la usiku wa Muungano lilifanyika Tarehe 25.04.2024 katika Ukumbi wa Community Centre kuanzia saa 9.30 mchana hadi saa 6.00 usiku wa kuamkia Tarehe 26.04.2024. katika usiku huo shughuli mbalimbali zilifanyika kama ifuatavyo.
6.1 MAONESHO YA VYAKULA NA VITU VYA ASILI.
Kikundi cha Umoja Nyamiaga kilionesho vitu mbalimbali vya Asili vilivyokuwa vinatumika kabla ya Muungano kama sahami, vyungu vya kupikia, vifaa vya kuchotea maji, kusaga unga kwa kutumia jiwe na vitu vya asili vilivyotumika zamani.
6.2 KUIMBA NYIMBO ZA TAIFA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ziliimbwa kama ishara ya ufunguzi wa Tamasha la usiku wa Muungano wa Tanzania.
6.3 DUA YANA SALA YA KULIOMBEA TAIFA
Viongozi mbalimbali wa dini walipewa nafasi ya kuliombea Taifa kwa Mwenyezi Mungu ili kuliepusha Taifa na watu wake katika majanga mbalimbali. Aidha Viongozi hao pia walimwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan na Wasaidizi wake ili waweze kuwatumikia Watanzania na Taifa bila kikwazo chochote
6.3 HOTUBA YA MHE. MKUU WA WILAYA
Mhe. Mkuu wa Wilaya aliwahutubia Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Ngara kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuliwezesha Taifa Letu kufikia mafanikio yaliyopo tangu Muungano wa Tanzania ulipozaliwa. Alielezea sababu za kuwepo kwa Muungano, mafanikio ya Muungano pamoja na kuwasisitiza Wananchi matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira. Alimalizia Hotuba yake kwa kueleza shughuli mbalimbali zilizofanyika ngazi ya Wilaya wakati wa Maadhimisho ya miaka 69 ya Muungano wa Tanzania.
6.4: BURUDANI VYAKULA NA VIBURUDISHO
Katika Maadhimisho hayo Vikundi mbalimbali vya burudani, Kwaya na Wasanii viliweza kutumbuiza Viongozi na Wananchi waliohudhuria usiku wa maadhimisho ya Muungano. Aidha kiliandaliwa chakula na vinywaji kwa Viongozi na Wananchi ambao walihudhuria usiku huo.
6.5: KUTAZAMA MUBASHARA HOTUBA YA MHE. RAIS WA MUUNGANO
Ili kutazama Mubashara hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wilaya ya Ngara iliandaa projector tatu zilizowekwa ndani nan je ya Ukumbi wa Community Centre. Majira ya saa 3.00 usiku hadi saa 3.27 usiku Viongozi na Wananchi waliohudhuria usiku wa Maadhimisho ya Muungano waliweza kutazama mubashara Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6.6: BURUDANI NA KUPIGA FATAKI
Ilipofika majira ya saa 6.00 usiku wa kuamkia Tarehe 26.04.2024 Viongozi na Wananchi waliohudhuria usiku wa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanzania waliimba Wimbo wa Taifa. Aidha fataki zilipigwa kama ishara ya kupokea miaka 60 ya Muungano. Burudani mbalimbali zilifuata kabla Mhe. Mkuu wa Wilaya kuhitimisha kilele cha usiku wa Muungano kwa maneno ya shukrani kwa Wananchi na Viongozi kwa jinsi walivyoshiriki maadhimisho hayo.
7.0: MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Kuendelea Kuenzi Muungano wetu kwa viongozi wa wananchi kufika kusaini kitabu cha kumbukumbu.
Ushirikiano wa Viongozi na Wananchi zoezi la upandaji miti ili kuendelea kuhifadhi Mazingira ili kulinda uoto na kusaidia upatikanaji wa mvua,
Wananchi kuanza kuelewa dhana ya nishati mbadala hasa matumizi ya gesi badala ya mkaa.
Wananchi hasa vijana kuelewa umuhimu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia maadhimisho ya miaka 60 ya muungano
wananchi na viongozi kuendelea kushiriki zoezi la usafi wa mazingira ili kuendelea kulinda afya za wananchi na mazingira yetu kwa ujumla
8:0 HITIMISHO.
Natumia fursa hii kushukuru uongozi wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa maelekezo ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano. hakika Wananchi na Viongozi wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ambapo wananchi wa Wilaya ya Ngara wamepata kujua umuhimu wa Muungano wa Tanzania.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa