- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA
Mhe. Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara, amekutana na Cde. Kauthari Yassin Chamani - Mwenyekiti wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama (Mkoa wa Kagera) pamoja na Cde. Godfrey John Wagahe - Mwenyekiti wa Taasisi hiyo (Wilaya) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo ngazi ya Wilaya kwa lengo la kujitambulisha na kueleza majukumu ya Kamati hiyo.
Kamati ya Mtetezi wa Mama ngazi ya Wilaya inatarajiwa kuunda Kamati ngazi ya Kata na kuanza majukumu ya kueleza mafanikio ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi hiki cha miaka mitatu akiwa madarakani.
Aidha, Mhe Col Mathias Kahabi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon Kimilike wameeleza mafanikio mengi yaliyofanyika na Serikali ya awamu ya Sita Wilayani Ngara ambapo zaidi ya Shs bilioni 38.7 zimetumwa ndani ya miaka mitatu na imetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Sekta za afya, Elimu, Maji, Barabara na Umeme. Kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Ngara Mhe DC Kahabi amemshukuru na kumpongeza sana Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutuma fedha ya kutekeleza miradi na kuahidi kutomwangusha Mhe Rais katika usimamizi wa miradi akishirikiana na Kamati ya Usalama ya Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Taasisi za Serikali Wilayani Ngara, Wataalam wa Halmashauri na Baraza la Madiwani wakiongozwa na Mhe Wilbard Bambara - Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Viongozi wa Taasisi ya mtetezi w a mama wakiwa na Col.Mathias J. Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara.
Kazi iendelee.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa