- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Mhe. Col Mathias Julius Kahabi anapenda kuwatangazia Viongozi na Wananchi wote kushirikiana pamoja kuhakikisha hakuna vitendo vya uchomaji moto hovyo vinaweza kufanywa na watu wachache wenye nia ovu ya kuharibu mazingira, uoto wa asili na hivyo kupelekea uharibifu mkubwa wa mashamba ya miti na mazao mbalimbali ya Wananchi na Jamii kwa ujumla.
Mhe Mkuu wa wilaya huyo amewaagiza Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hili la kudhibiti matukio na vitendo vya uchomaji moto hovyo, kuwa havitokei katika maeneo yao.
Mtendaji yeyote ambaye moto utabainika kutokea katika eneo lake atawajibika kuwabaini na kuwachukulia hatua wahusika.
Aidha, Utaratibu wa kutuma taarifa kwa Mkuu wa wilaya kila Ijumaa uko pale pale kwa Watendaji wote wa Kata.
Kauli Mbiu ya Mazingira 2024 "Urejeshwaji wa Ardhi Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame"
Shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji Kwa uadilifu
Kazi inaendelea....
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa