- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.22, kwa ajili ya kutengeneza barabara zenye urefu wa kilomita 659 katika halmashauri hiyo, katika mwaka wa fedha 2018/19.
Meneja wa TARURA wilayani Ngara Vincent Subira Manyama, alisema hayo ofisni kwake Disemba 19,2018, kwamba barabara hizo zitarahisisha mawasiliano ya kijamii na kuchochea maendeleo katika kata 22 wilayani Ngara
“Kati ya fedha hizo Sh1.12 bilioni zitatumika kwenye Matengenezo ya barabara zenye urefu huo na Sh102.48 milioni ni fedha za usimamizi, utawala na upembuzi yakinifu wa mtandao wa barabara.” Alisema Manyama
Alisema barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha lami katika mamlaka ya mji mdogo wa Ngara, ikiwemo ya Mubinyange kuelekea Ikulu ndogo wilayani Ngara na nyingine zitawekewa changarawe baada ya kuthibitisha bora wake.
“Mikataba sita iliyosainiwa imegawanyika, ikiwemo ya kuweka changarawe kuzisafisha ili zirejee katika hali ya kawaida, na nyingine zitawekewa madaraja ili ziweze kuharakisha mawasiliano vijijini na mijini” Alisema Manyama.
Pamoja na hayo, wananchi wamewaomba wakandarasi wanaotengeneza barabara hizo, wafanye utaratibu wa kuziwekea changarawe na kuziba mitaro, ili maji yasituhame katika barabara hizo na kupelekea kukwama kwa magari kwenye maeneo yao.
Amewataka wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuzitunza barabara hizo kwani serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo yake, huku akiwaomba viongozi ngazi zote kuwachukulia hatua wale wote wanaohujumu miundombinu hiyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa