- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tatizo la ukosefu wa matundu ya vyoo katika shule ya sekondari ya Kabanga Wilayani Ngara, uliokuwa unasababisha wanafunzi wa shule hiyo, kuchafua mazingira kwa kujisaidia vichakani, umepata muarobaini baada ya kufadhiliwa matundu ya vyoo 12 na tanki la maji, vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 47.
Ufadhili huo ulitolewa na DKT. Suzanne kutoka nchini Uingereza, ambaye alitembelea shule hiyo mwaka 2014, na kukuta upungufu wa wa matundu ya vyoo uliokuwa ukisababisha wanafunzi kuangaika kupata huduma hiyo.
Dr. Suzanne amesema amepata kiasi hicho kwa kufanya harambee kupitia shule rafiki na Kabanga Sekondari ya Les Beaucamps ya Uingereza, nchini Uingereza na kufanikiwa kupata kiasi hicho, huku akiwashukuru uongezi wa shule kwa kusimamia shughuli hiyo.
Dkt. Suzan Wilson kutoka Uingereza amesema "Maendeleo ni Afya na kwamba Maji na Afya ni Maendeleo" hivyo watumie maji na vyoo kutunza Afya zao wakijikita kusoma kwa juhudi na maarifa na kwambachangamoto nyingine zitatatuliwa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, akikagua miundombinu hiyo, baada ya kuizindua na kuikabidhi katika uongozi wa Shule, ameutaka uongozi huo kuitunza miundombinu hiyo.
Amesema kitu ambacho mzazi anaweza kumpatia mtoto wake kama urithi hapa duniani ni elimu hiyvo, akaitaka jamii ya wanangara kuwapeleka watoto wao shuleni, ili waweze kunufaika na elimu inayotolewa na serikali bila malipo iweze kuwafaidia katika maisha yao.
Akikabidhi mradi huo Januari 17, 2019; Mratibu wa Shirika la Tumanini Fund wilayani Ngara, Ndugu Alex Nyamkara, amesema ujenzi wa vyoo vitatu vyenye matundu 12, utapunguza magonjwa ya mlipuko na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi kitaaluma.
"Mazingira ya kupata taaluma yanahitaji usalama wa kujisitiri hivyo katika vyoo vilivyojengwa kimetengwa chumba maalum kwa wanafunzi wa kike wanaopatwa na changamoto ya hedhi kila mwezi darasani" Amesema Nyamkara.
Amesema Ombi la Tanki la maji lenye thamani ya Shilingi milioni 6, na vyoo vilivyogharimu Shilingi milioni 41, lilitolewa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi. Honoratha Chitanda, baada ya ujumbe wa shule rafiki ya Les Beaucamps ya Uingereza kutembelea Kabanga mwaka 2014.
Mkuu wa shule ya sekondari Kabanga Projestus Katura, amesema shule hiyo, ilianzishwa mwaka 1990; ikiwa ya kwanza wilayani Ngara, kumilikiwa na serikali, ina wanafunzi 1,133, kati yao wasichana 630 na wavulana 503, wakifundishwa na walimu 35.
Ameishukuru Tumaini Fund kwa ufadhili wa miundombinu hiyo, pamoja na wa kompyuta walizofadhiliwa miaka iliyopita, ingawa bado shule hiyo iana changamoto ya uhaba wa maji, vyumba vya madarasa, Bweni na kuomba kuboreshewa tanki lililopo la kuvuna maji ya mvua.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa