- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ikiwa ni mfululizo mwaka huu Tena Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni mojawapo ya washiriki wa michezo ya watumishi Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) kitaifa Iliyofanyika Jijini Dodoma kuanzia Tarehe 18/11 Hadi 30/11/2023
Leo tarehe 6/11/2023 washiriki wa Michezo hiyo wamefika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Kwa ajili ya kukabidhi Medali za dhahabu, Shaba na Fedha.
Pia cheti Cha Ushiriki wa Mashindano hayo na cheti Cha Mchezaji Mwenye nidhamu.
Taarifa imetolewa na mratibu wa michezo Wilaya ya Ngara kuwa timu iliweza kupata Medali 3 Kwa ajili ya Riadha Mbio Mita 100 nafasi 2 kitaifa Mita 200 nafasi ya 3 kitaifa ,na Mita 800 2 kitaifa
Aidha Mbio tumeweza kufikia hatua ya fainali Mita 1500 na 3000 nusu fainali Mita 400 .
Katika mchezo wa karata Halmashauri ya Ngara ilikuwa ya 4 kitaifa baada ya kufungwa katika kutafuta mshindi wa tatu kitaifa dhidi ya Halmashauri ya Bahi 2 Kwa 1 . Mchezo wa poolteble Ngara iliishia hatua ya robo fainali.
Mideli hizo na cheti zimekabidhiwa Kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike katika kikao Cha Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri (CMT)
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike amewapongeza sana wanamichezo hao Kwa kuhakikisha wanashindana na kurudi na medali aidha amewataka mwakani kuanza maandalizi mapema ili kushiriki na michezo mingine pia amesisitiza kuweka bajeti kama ilikuwa mwaka huu.
Taarifa fupi ikisomwa katika kikao Cha wataalam ( CMT)
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa