- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wataalamu na wadau wote wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya mazignira, ili kuepeusha madhara yananyoweza kutokea kutokana na kukata miti ovyo, kuchoma mistu na kuaribu vyanzo vya maji.
Akiongea na wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge, wakati wa siku ya kilele cha wiki ya Mazingira June 05, 2018, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Rulrnge Ndugu Moris Mombia, amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutunza mazingira.
“Tunaaribu vyanzo vya maji, uonto wa asili matokeo yake; maji yatakauka, miti itaisha tutakuwa na jangwa, kwa hiyo hata huo mkaa hamtauchoma, matanuru ya matofari mtakosa kuni za kuchomea tofali, na wala maji ya kufyatulia tofali. Alisema ndugu Moris.
Amewataka kuacha kabisa kutumia miti ya asili kuchomea mkaa, badala yake watumie miti ya kupanda kama vile mikaliptusi na pine, huku akiwasisitiza kupanda miti kila wanapokata miti ya kuchoma mkaa.
Naye Kaimu Afisa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Zawadi Waziri, amewaambia wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji wa mchanga, kuchoma tofari na mkaa kujiunga katika vikundi ili waweze kupata leseni na hivi watambulike kisheria.
Amewataka kutumia nishati mbadala kama vile kutumia gesi, na majiko ya kisasa kwa ajili ya kuzuia uaribufu zaidi wa mazingira.
Wiki ya mazinigira imehitimishwa rasmi June 06, 2018, katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge, kwa kufanya usafi katika hospitali ya Rulenge, kutoa elimu ya mazingira kwa wachoma mkaa, wachoma tofali, wachamba mchanga na mama lishe.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa