- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watendaji wa kata na wa vijiji wilayani Ngara wametakiwa kutoa taarifa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya za mtu, atakayejiandikisha kupata kitambulisha cha taifa wakati si raia wa Tanzania, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya, kilichofanyika Machi 02, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya.
Amewataka watendaji wa kata na wa vijiji kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi, ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha; huku akiwaomba kutoa taarifa za kweli za mtu atakayetaka kujiandikisha wakati ni muhamiaji.
“Nimepata taarifa kwamba baadhi ya viongozi wa vijiji wanapokea fedha, ili kuwaandikisha wahamiaji; nitahakikisha taasisi zinazohusika zinawafuatilia na wakigudulika hatua sitahiki zitachukuliwa dhidi yao.” Alisema Lt. Col. Mntenjele.
Amesema suala la vitambulisho ni la kitaifa, hivyo viongozi wote wanawajibika kulisimamia kwa karibu; huku wakizingatia misingi na maadili katika utendaji wao, ili wahakikishe wanaoandikishwa wana sifa za kupata vitambulisho hivyo.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Aidan John Bahama, hivi karibuni amewasimamisha wafanyakazi wanne (04) wanaowaandikisha wananchi kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifa, baada ya kukiuka maadili, kanuni na taratibu za kuifanya kazi hiyo.
Amewataka waliobaki kazini kufanyakazi kwa uadilifu na bidii kubwa ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati; na kuongeza kuwa atakayekiuka utaratibu huo itabidi akae pembeni.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa