- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwapa ushirikiano wafanyakazi wa afya waliohudhuria mafunzo ya kupambana na magonjwa ya mlipuko, ili kwa kutumia elimu hiyo waweze kuyathibiti magonjwa hayo.
Wito huo umetolewa na Afisa Afya wa Mkoa wa Kageara Ndugu Nelson Rumbeli, wakati wa mafunzo yatakayodumu kwa siku nne tangu Novemba 5-8, 2018, ya kumpambana na magonjwa ya mlipuko yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri na kujumuisha wadau wapatao 400.
“Wawapokee wahudumu wetu wa afya na wawapatie ushirikiano kwa namna moja au nyingine, kwa sababu wamepata mafunzo mazuri; kimsingi kama wakiwapa ushikirikiano wa kutosha wanaweza kuwasaidia huko mbele ya safari.” alisema Ndugu Rumbeli
Amewataka wananchi wayatumie mafunzo hayo kama fursa, ili waweze kupambana na magonjwa ya mlipuko, ambayo kimsingi yanarudisha maendeleo ya wananchi nyuma kiuchumi na hata kiafya.
Wameazimia kutoa mafunzo haya katika Halmashauri za Wilaya ya za Ngara na Missenyi kwanza, kwa sababu ziko katika hatari ya kupata magonjwa hayo kwa sababu ya mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda, ambako kuna milipuko ya magonjwa ya Ebola na polio.
Katika mkoa wa Kagera wameanza na Halmashauri mbili za Ngara na Missenyi, lakini nia ya mkoa nikuendelea kutafuta wadau wengine wanaoweza kutufadhili, ili tuwe na uwezo wa kuwa na mfumo wa namna hiyo katika ngazi ya jamii katika Halmashauri zote za mkoa wa kagera.
Kwa hiyo ofisi ya Afya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo aliyowataja kuwa ni JSI kwa kupitia USAD, waliona ni busara kufanya mafunzo ya jinsi ya kuzuia magonjwa ya mlipuko katika ngazi ya jamii.
Mkoa umekuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya, lakini kumekuwepo na mapungufu katika kufuatilia magonjwa ngazi ya jamii, kwa maana ya kupata tetesi za kuwepo kwa magonjwa hayo, kwenye maeneo ya vijiiji au maeneo ya jamii.
Ndugu Rumbeli amesema kwamba hafua hii, inalenga kuweka mfumo katika ngazi ya jamii, ambao unaweza kusaidia kupata taarifa au tetesi mbalimbali za magonjwa ya milipuko katika ngazi ya jamii, na baadae katika ngazi ya mkoa.
Kimsingi ni itaji la kisheria; ukiagalia kanuni za afya za kimataifa wanahitaji kuwa na mfumo wa namna hiyo, ili wawe na uwezo wa kufuatilia magonjwa ya mlipuko katika nagazi za jamii, kwa ajili ya kupata taarifa za zinazohusiana na magonjwa ya mlipuko.
“Kwa hiyo tumeona njia nzuri ya kufuatilia magonjwa ya milipuko ni kutoa elimu kwa viongozi wa afya ngazi ya jamii, ili tuweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka, na hivyo kurahisisha ufuatiliaji wa kuzuia yasienee zaidi na kusababisha maafa kwa wananchi wetu.” Alisema Ndugu Rumbeli.
Amesema mafunzo haya yanawahusisha waheshimiwa madiwani, kwa sababu wao ndiyo watekelezaji wakuu wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020, kuongeza kwamba ibara ya 48 hadi ya 50 yapo amelekezo yanayohusiana na idara ya afya.
Kwa hiyo ni vema wakafahamu kwamba katika shughuli hizi za afya, katika kufuatilia magonjwa tunatekeleza ilani hiyo; lakini pia wao ndo wanafanyakazi na wananchi moja kwa moja kupitia mikutano iliyorasmi na isiyo rasimi ukilinganisha na wafanyakazi wa afya.
Pia mafunzo hayo, yamewashirikisha watendaji wa kata, kwani ndiyo wanaosimamia shughuli za kila siku za serikali ngazi ya kata, huku wagani wa kilimo na mifugo wameshikishwa, kwa sababu yapo magonjwa yanayoambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa