- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Taasisi ya Tumain Fund katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imefadhili vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu pamoja na madawati 30, katika shule ya msingi Kihinga wilayani humo, vilivyoaribika kufuatia mlipuko wa bomu Novemba 2017, kwa gharima ya shilingi milioni 76.
Mratibu wa taasisi hiyo Alex Nyamkara na Mwenyekiti wa mfuko huo Dkt Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza, wamekabidhi miundombinu hiyo Januari 19, 2019 kwa uongozi wa shule hiyo baada ya mlipuko huo kuaribu vyumba vya madarasa vinne, wanafunzi watano kufariki dunia na wengine 43 kujeruhiwa.
Nyamkara amesema pamoja na ujenzi wa vyumba hivyo, wakati wa tukio hilo Tumaini Fund, ilitoa msaada wa matibabu kwa waadhirika, yaliyogharimu shilingi milioni 6 kwa wanafunzi, waliolazwa katika Hospitali ya Rulenge wilayani Ngara.
“Msaada mwingine wanafunzi wote wa shule hii, walipewa vifaa vya kujifunzia darasani, ambapo majeruhi walipatiwa sare za shule na vifaa vya kujifunzia, huku familia zilizopoteza watoto, tuliwapa pole ya vyakula” Alisema Nyamkara.
Dkt Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza, amesema wanafunzi watatu waliopata ulemavu wa kudumu atarudi hapa nchini kuwaletea vifaa maalumu vya kutumia, kulingana na ulemavu wao, ili waweze kuendelea na masomo yao.
Wanafunzi waliopata ulemavu wa kudumu ni Emanuel Hilali, Melania Razalo, ambapo walipofuka macho, na kuwekewa ya bandia katika Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro, ambapo Domina Wabandi alibaki na uoni hafifu.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, ameitaka jamii ya shule hiyo kutunza miundombinu hiyo, na kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama katika kijiji hicho, ili tukio hilo lisijitokeze tena.
Shule hiyo inao wanafunzi 882 kati yao wavulana ni 452 na wasichana 430, ambapo inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo 20, nyumba za walimu 10, vyumba vya madarasa vinane, huku ikihitaji umeme, kompyuta na bendera ya Taifa. ujenzi wa miundombinu hiyo imefadhiliwa na Dkt Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa