- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Fedha zitaendelea kuwa kidogo ongezeko la wanafunzi limekuwa mara mbili ya uwezo wa miundombinu iliyopo, lazima tutumie fedha kidogo zinazokuja kuboresha zaidi upatikanaji wa miundombinu katika shule zetu.” Alisema Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti.
Brig. Jen. Gaguti alitoa rai hiyo Novemba 21, 2018 wakati wa ziara yake ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, ili kuangalia utayari wa mkoa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, awali na wa darasa la kwanza mwaka wa masomo 2019.
“Kuja kwangu hapa sitarajii kujibu hoja yoyote iliyojitokeza, ispokuwa nikirudi nitafanya tathimini na ikiwezekana tutaitana viongozi wote wa mkoa, ili tushiriki katika kikao cha pamoja kuona nini kifanyike, ili lengo liweze kutimia.” Alisema Ndugu Gaguti.
Alisema anafahamu kwamba mpango wa elimu bila malipo kwa wanafunzi, umeogeza Baraka la kuwa na kiasi kikubwa cha wanafunzi, ikilinganishwa na idadi ya wanaohitimu darasa la saba; huku akisisitiza kwamba dhamira yake ni kuona jinsi Halmashauri, ilivyojipanga kukabiliana na ongezeko hilo.
Mkoa usingependa kuona muhula wa masomo mwaka 2019, unaanza huku wanafunzi wakiwa na changamoto ya miundombinu ya kupata elimu; kwake hilo ndo kubwa na akatoa rai ya kuhakikisha halitokei mkaoni humo.
Ameutaka uongozi wa Wilaya ya Ngara kuweka mikakati halisia ya kuhakikisha miundombinu inapatikana, ili wilaya na mkoa kwa ujumla uweze kufikia lengo la kuendelea kubaki katika kiwango cha ubora wa elimu kinachohitajika.
Katika taarifa ya sekta ya elimu iliyowakisilishwa kwa Mkuu wa Mkoa, imeonyesha kwamba shule ya msingi ina wanafunzi 5065 waliohitimu darasa la saba mwaka 2018, na maoteo ni 23130 watakaingia awali na darasa la kwanza mwaka 2019.
Kwa upande wa shule za sekondari katika Wilaya ya Ngara, takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2018, wamehitimu kidato cha nne wanafunzi 1730, na wanatarajia uenda idadi hiyo ikaongeza mara mbili.
Takwimu za taarifa hiyo zmeonyesha kwamba, ili kukidhi haja shule za sekondari wilayani humo, vinahitajika vyumba vya madarasa viapatavyo 106 ambapo mapungufu ni vyumba 45, maabara zipo 66 zinapungua 22, ambapo matundu ya vyoo yapo 180 na yanapungua matundu 60.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa