- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wameagizwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha, ili waweze kujipatia mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na biashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe. Erick Nkilamachumu, ametoa wito huo ofisini kwake wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi Machi 14, 2018.
Amesema kwamba ni bahati kupata mvua hizi, kwani miaka miwili iliyopita uzalishaji ulikuwa hafifu, kwa sababu ya ukame, hivyo ni vema wakatumia fursa hii kuzalisha zaidi.
Amewaomba wananchi kutunza chakula walichokipata msimu huu, badala ya kukiuza chote na baadae wakaadhirika kwa njaa.
“Tumepata mahindi na maharage ya kutosha msimu huu wa 2018, kwa hiyo niombe mavuno haya tusiyauze yote, halafu tukaangaika kwa kukosa chakula huko mbeleni.” Amesema Mhe. Nkilamachumu.
Aidha, amewaomba wananchi kutoa taarifa ya kitu kisicho cha kawaida, ili kuepuka hasara ya kulipukiwa na mabom, kama ilivyotokea mwaka jana kijijini Kihinga.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa