- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kutumia muda, juhudi na nguvu nyingi katika kujisomea, kwani ndiyo azima pekee iliyowaweka shuleni.
Afisaekimu Taaluma wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Jared Nyaonge, ameyasema hayo Machi 23, 2018, wakati wa mahafali ya pili ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Muyenzi.
“Mnatumia nguvu nyingi kujiandaa kwa michezo ya sherehe za mahafali, vizuri, lakini tumieni juhudi na nguvu kama hizo katika kujifunza; ninaamani mtafanikiwa sana.” Alisema ndugu Nyaonge.
Amewataka wanafunzi hao kushirikiana katika kujifunza, na kutoa ushirikiano huo kwa walimu wao, ili waweze kufaulu vizuri mitihani yao, na kufuta kabisa daraja la nne na ziro.
Amewashauri kuendelea na nidhamu, ambayo anaamini ndiyo iliyowafikisha walipo, na kuongeza kwamba, maisha yanaendelea baada ya kukamilisha masomo yao shuleni Muyenzi.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Muyenzi, amewataka wazazi kuwasaidia watoto wao, kujua kozi watakazosoma elimu ya juu, ili wanapoomba vyuo wawe tayari wanajua, wanchokihitaji katika maisha yao.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa