- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisaelimu Kata 22 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kutumia pikipiki walizopata kuinua kiwango cha elimu katika kata zao, ili wilaya ipande kielimu na kufikia nafasi ya kwanza kimkoa na hata kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameyasema hayo Septemba 08, 2018 katika ofisizya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara alipokuwa akiwakabidhi pikipiki 22 watendaji wa kata 22 katika Halmashauri hiyo.
“Ni mategemeo ya serikali kwamba mtaongeza jitihada za kusimamia elimu; mkoa wa Kagera kwa ujumla wake wilaya ya ngara ikiwemo, imekuwa na sifa nzuri ya kufanya vizuri katika masomo ya shule za msingi na za sekondari.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Amewambia Maafisaelimu hao kuwa yeye kama mkuu wa mkoa anapowakabidhi pikipiki hizo anatarajio kuona ubora wa elimu katika mkoa wa Kagera unaongezeka; na kuogeza kwamba kuanzia mwaka 2019 mkoa utachukua nafasi ya kwanza katika kufaulu mitihani ya darasa la saba kitaifa.
Kwa mkuu wa mkoa huyo kikubwa ni walimu kusimamia na kufuata taratibu, kanuni na maadili ya kazi ya ualimu, likiwemo suala la utoaji adhabu kwa wanafunzi, na kudai kwamba asingependa kuona tatizo lililotokea katika Manispaa ya Bukoba litokee tena katika Mkoa wa Kagera.
Amesema walimu wamepewa dhamana kubwa ya kusimamia elimiu na kuhakikisha kwamba mifumo ya elimu, iliyowekwa na serikali inasimamiwa na kuzingatiwa vizuri; huku akiwataka maafisaelimu hao kutumia vyombo hivyo kuthibiti utoro wa wananfunzi katika shule zote za msingi Wilayani.
“Tumepewa vifaa hivi tuvitunze vifanye kazi leo, vifanye kazi kesho na siku zote zijazo, ili elimu iendelee kuwa bora siyo katika mkoa wa Kagera tu, bali katika taifa zima.” Alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama amesema kwamba pikipki hizo si za kufanya kazi binafsi, bali zimetolewa na serikali kwa ajili ya kwenda kufanya ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ya elimu katika kata zao.
Mkuu wa Kagera amekabidhi pikipiki 22 kwa Maafisaelimu Kata 22 Septemba 08, 2018 wakati alipokuwa katika ziara ya kujitambulisha kwa watendaji wa mkoa wa Kagera, ili aweze kujua matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Katika Ziara yake Wilayani Ngara alipata nafasi ya kutembelea mradi wa afya katika kata ya Mabawe, ambapo aliongea na wananchi, kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha Ngara Coffee, kuongea na watumishi wa Halmashauri, wafanyabiashara na kuhitimisha ziara yake kwa kukabidhi pikipiki kwa maafisaelimu 22.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa