- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi mkoani Kagera wametakiwa kuitunza historia ya kufanya vizuri kitaaluma kwa kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo ya kadiri ya taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali na kuongeza miundombinu inayopungua katika taasisi za elimu mkoani humo.
Hayo ni kwa mujibu wa Afisaelimu wa Mkoa wa Kagera Ndugu Aloyse Kamamba Aprili 04, 2019 wakati akiongea na mwandishi wa habari hii kwamba mkoa huu ni mmoja kati ya mikoa inayofanya vizuri kitaaluma.
“Mkoa wa Kagera ni mmoja wa mikoa inayofanya vizuri kitaaluma tusiiharibu historia hiyo natunaweza tukaiaribu historia hiyo endapo watoto wayendelea kutoroka, au miundombinu haitakuwa ya kutoshereza.” Alisema Ndugu Kamamba.
Akizungumzi matokeo kwa miaka miwili mfululizo amesema kwamba mkoa wa Kagera, umefanya vizuri, kwani umeshika nafasi ya 08, kati ya mikoa 31 ikiwemo ya Tanzania visiwani katika matokeo ya darasa la saba kitaifa mwaka 2018.
Mwaka 2017 mkoa ulishika nafasi ya 09 kwa hiyo; umepanda nafasi moja, huku akisema kwamba kuna baadhi ya Halmashauri ambazo hazikutimiza wajibu wake vizuri kama Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi aliyodai kuwa “haikututendea haki uwajibikaji wake ulikuwa ni hafifu.”
Ameitaka jamii mkoani humo kushiriki katika ujenzi wa miundombinu inayopungua shuleni msingi na sekondari huku akiwataka wazazi kuwafuatilia watoto wao wanaporudi toka shuleni ili wajiridhishe na maendeleo yao kimasomo.
“Tusiwaache watoto wanajipeleka shuleni na kujirudisha tu, lakini walau wanapotoka shuleni, wazazi wahakikishe wanajiridhisha kwa kuaangalia walichokifanya watoto wao shuelni kama wanaendelea vizuri na kama wamehudhuria shuleni.” Alisisitiza Ndugu Kamamba.
Aidha, amewasihi wazazi, kuhakikisha kwamba watoto wanapata chakula wawapo shuleni na kwani tumbo lililowazi linamfanya mtoto hasishiriki vizuri masomo yake; hivyo, amewaomba wazazi, wahakikishe watoto wao wanapata chakula wanapokuwa shuleni.
Kwa upande wa wasimamizi wa masuala ya elimu ambao ni wanasiasa wakiongozwa na Mh. mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa huo, amewaomba waendelee kusaidia, ili wahakikisha miundombinu inatosheleza katika taasisi za elimu.
katika kuhakikisha kwamba historia ya kufanya vizuri kitaaluma inadumu, amewataka maafisaelimu katika wilaya zote wafuatilie na kusimamia ufundishaji wa walimu, ili mkoa uendelee kufanya vizuri.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa