- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu. inayojengwa katika shule ya sekondari ya Murusagamba, na kuwataka wahusika kuitunza, ili iwe na tija kwa walengwa.
Ndugu Bahama amesema hayo Aprili 01, 2019 shuleni hapo, alipotembelea eneo hili, ili kujiridhisha na maendeleo ya mradi huo, matumizi ya mali na fedha, iliyotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili, bweni, bwalo na jiko pamoja na maktaba.
Amesema kwamba juhudi zinzoendelea katika ujenzi wa mradi huo unaridhishwa kwa sababu kwa muda mfupi tayari wanapaua vyumba viwili vya madarasa, bwalo limefikia hatua nzuri, na bweni limefikia usawa wa lenta.
“Wito wangu kwa walimu , wanafunzi na wananchi wanaozunguka mradi huu, mali zinazoletwa kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu hii, itunzwe vizuri kwa sababu ni fedha nyingi za serikali zilizowekezwa hapa, itakuwa si busara zikitumiwa tofauti na malengo yalikusudiwa.” Alisema Ndugu Bahama.
Lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuona miundo mbinu hiyo, imekamilika ili iweze kutatua changamoto za upungufu wa mabweni, makitaba, pamoja na bwalo katika taasisi hiyo; huku ikitoa nafasi za masomo kwa vijana wengi zaidi katika shule hiyo.
Aidha, amewapongenza wasimamizi wa majengo hayo, ambao amewataja kuwa ni walimu wa idara ya ujenzi, kamati ya ujenzi na watu wote wanaofanyakazi katika mradi huo, kwa jitihada wanazozionyesha katika kuhakikisha majengo hayo, yanakamilika kwa wakati.
Serikali iliipatia shilingi milioni 265, shule ya sekondari ya Murusagamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa ajili ya kujenga Bweni, Maktaba, Bwalo na jiko, pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo, ambayo ina kidato cha kwanza hadi cha sita.
“Fedha hizi zimegawanyika katika miuondombinu ifuatayo; shilingi milioni 100 zitajenga Bwalo, shilingi milioni 75 zitajenga Bweni, shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga Maktaba, na shilingi milioni 40 zitatumika kujenga vyumba 02 vya madarasa.” Alisema Ndugu Bahama.
Miradi hiyo itatekelezwa kwa kutumia false akaunti, ambayo inatumika katika ujenzi wa miundombinu ya serikali katika shule za sekondari na za msingi, huku akisema wamafika shuleni kutoa elimu kwa kamati na Bodi ya shule namna ya kutumia fedha hiyo.
Idara ya elimu sekondari na timu ya wataalamu wa Halamashauri ya Wilaya ya Ngara watafanyakazi pamoja na kamati hiyo, kwa ajili ya kutoa ushauri na usimamizi wa kitaalamu pale watakapohitajika kufanyahivyo wako tayari.
Shule ya sekondari ya Murusagamba ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita; ambapo shule hiyo ina mchepuo wa masomo ya sayansi; na wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao ya ndani, kiwilaya, kimkoa na hata kitaifa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa