- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Ngara Ndugu George Rubagola, amewataka wajumbewa mkutano mkuu wa chama hicho, kuvuta subira wakati serikali inajipanga kutumafedha za miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2017/2018.
Mwenyekitiwa CCM Ndugu Rubagola ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa mkutano mkuu waCCM Wilaya uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya, kujadiliutkelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015.
Amesemamiradi mingi ya maendeleo imesimama kwa sababu fedha haikufika kwa wakati,ameitaja miradi hiyo kuwa ni kilimo, maji, elimu na afya na kuongeza kwambasubira na busara ni muhimu wakati fedha hiyo inafuatiliwa.
Aidha, wataalamuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wamebaini kuwa hadi kufikia Desemba 2017,miradi ya maendeleo ilitekelezwa kwa 34% tu katika mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Wamesema kuwamiradi hiyo ilikuwa ikiendelea vizuri na tisa (09) kati ya iliyokusudiwa inatarajiwakufunguliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru Aprili 14, 2018.
Mwenyekitiwa CCM amewashukuru wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya; na kuwaomba kuwaelimishawananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii; afya, elimu, kilimo na utaliiili wananchi hao waweze kujikwamua kiuchumi.
Baada yakujiridhisha kwamba miradi yote iliyopewa fedha ilikuwa ikiendelea vizuri,wajumbe wa mkutano huo waliipokea taarifa ya miradi ya maendeleo; hukuwakiwataka wananchi wilayani Ngara kuendelea na moyo wa kutaka kujileteamaendeleo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa