- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo ni siku ya Wanawake Duniani ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara,siku hii imeadhimishwa katika Mamlaka ya Mji mdogo Rulenge.Maadhimisho haya yameongozwa na kauli mbiu ya “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadae”.
Mgeni Rasmi wa Siku hii alikuwa Ndugu Issa Samma ambaye aliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ngara Ndugu Aidan Bahama. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara Ndugu Eric Nkilamachumu, Wakuu wa Idara ya Halmashuri ya Ngara,wadau mbalimbali wa Maendeleo akiwemo Meneji wa benki ya CRDB,Meneja benki ya NMB, Meneja TCRS na wadau wa taasisi nyinginezo.
Akifungua maadhimisho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Ngara aliieleza hadhara jitihada za Serikali katika kutoa fursa mbalimbali zinazokusudia kumwinua mwanamke kutoka kwenye hali duni ya uchumi. Mkurugenzi alieleza kuwa Halmashauri imeendelea na jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa asilimia kumi (10%) ya mapato yake kwa ajili ya kuwainua wanawake ingawa mwitikio wa wanawake bado hauridhishi.
“Tumieni fursa hii ya kukutana kwenu kwenye siku hii muhimu kupeana elimu na kuwafikishia elimu wale ambao bado wako gizani juu ya fursa mbalimbali za wanawake wanazoweza kuzipata kwa faida yao. Mfano ni asilimia ya fedha inayotolewa na Halmashauri ambapo wengi bado hawajajitokeza ili wanufaike nayo.Pia mkiondoa kuchukiana nyinyi kwa nyinyi,mkawa na uthubutu wa kuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo na mkaondoa ubinafsi basi usawa wa kimaendeleo na kijamii utawezekana. Ila yakikosekana hayo ni ngumu kwa mwanamke kujikwamua kama kauli mbiu inavyosema.”alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Ngara.
Naye mgeni Rasmi Ndugu Issa Samma katika hotuba yake aliwasisitiza wanawake katika kushirikiana na kupendana wao kwa wao kwanza maana ndio nguzo kuu za kufanikiwa.
“Pasipo na upendo hakuna maendeleo wala pasipo na ushirikiano hakuwezi kuwa na usawa kama mnavyosema kwenye kauli mbiu yenu”alisema Ndugu Issa Samma.
Katika maadhamisho haya,Wanawake wilayani Ngara walitembelea vituo viwili vya kulea watoto yatima na Wazee vya Karkuta na Malaika vya Rulenge ambapo walitoa mahitaji mbalimbali kwa watoto hao na wazee. Pamoja na yote mgeni Rasmi alitoa mchango wake kwa kikundi cha akina mama wa wilaya ya Ngara pamoja na mahitaji kwa vituo vilivyotembelewa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa