- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe.Ndaisaba George Ruhoro anawajulisha Wananchi wa kata ya Ngara Mjini kuwa kampuni ya kuchimba visima iliyosaini Mkataba na NGUWASA imeanza kazi rasmi ya uchimbaji wa visima hivyo.
Lengo kuu la uchimbaji wa visima viwili vipya ni kuongeza uzalishaji wa Maji safi yatakayowezesha upatikanaji wa maji maeneo ya Nyamiaga na maeneo mengine yanayozunguka Mji wa Ngara mjini.
Mhe.Mbunge anaendelea kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na *Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan*, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali Kwa Wananchi wa Jimbo la Ngara.
Mhe. Mbunge anapenda kumpongeza Mhe Staford Kennedy Festo Diwani wa Kata ya Ngara mjini kwa kuendelea kusimamia vema Miradi ya Wananchi katika namna ambayo inaridhisha kabisa ikiwemo usimamizi wa tbha Mradi huu ambapo Diwani huyu ameendelea kuusimamia mradi huu na alishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa uchimbaji wa visima hivi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa